NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, MWANZA
MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella, amewaasa madaktari kuzingatia mafunzo wanayopewa kuhusu namna ya kufanya tathmini ya ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi ili kuchangia kulinda nguvukazi ya taifa iliyo muhimu katika kujenga uchumi wa viwanda na hatimaye kuleta maendeleo ya taifa.
Mhe. Mongella ameyasema hayo hivi karibuni wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo madaktari na watoa huduma za afya kutoka mikoa sita ya kanda ya ziwa kuhusu namna ya kufanya tathmini ya ulemavu kwa mfanyakazi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi - WCF,  mjini Mwanza ambapo madaktari wapatao 100 kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Mara, Kagera, Shinyanga na Simiyu wanapata elimu ya masuala mbalimbali na kujenga ujuzi wa kufanya tathmini za ulemavu kutokana na ajali au magonjwa yatokanayo na kazi.
Mhe. Mkuu wa Mkoa alibainisha kuwa wafanyakazi ni rasilimali muhimu katika kujenga uchumi wa viwanda ambapo Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli inatilia mkazo juu ya mazingira salama ya kazi na haki stahiki za Wafanyakazi ziweze kutambulika na kupatikana kwa wakati, na sehemu ya dhamana hiyo iko kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
“Hii ni mara ya tatu kwa kanda hii kupata mafunzo kama haya, hivyo ni dhahiri Mfuko umeweka umuhimu mkubwa  katika kuhakikisha wafanyakazi wanapata fidia stahiki na kwa wakati.
Kwahiyo niipongeze sana WCF na Serikali na pia niwaombe madaktari na watoa huduma za afya wazingatie mafunzo haya ya kitalaam ili kuwezesha wafanyakazi kupata haki zao stahiki pale wanapopata madhara wakati wakitekeleza wajibu wao wa kikazi” Alisema Mhe. Mongella.
Mkuu huyo wa Mkoa pia ameipongeza WCF kwa kuendelea kutanua wigo wa wataalamu wenye ujuzi wa kufanya tathmini za madhara iliyo sahihi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Anselim Peter, alisema Mfuko umeendelea kutoa mafunzo hayo maalum kwa madaktari katika kanda mbalimbali nchini ili kuwajengea uwezo na mpaka sasa idadi yao ni zaidi ya 850.
“Mafunzo haya ni muhimu sana katika utekelezaji wa shughuli za Mfuko, kwani ili mfanyakazi aweze kulipwa fidia ni lazima daktari afanye tathmini na kubaini kiwango cha ulemavu alichopata mfanyakazi kutokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi. Hivyo mafunzo haya kwa madaktari yatasaidia zaidi kuboresha huduma zetu kwa wanachama wetu.” Alifafanua Bw. Peter.
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella, akihutubia madaktari na watoa huduma za afya kutoka mikoa sita ya kanda ya ziwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo wa namna ya kufanya tathmini ya ulemavu kwa mfanyakazi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kwenye ukumbi wa chuo cha BoT jijini Mwanza. 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo. Wakwazna kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu WCF, Bw. Anselim Peter, na katikati ni Kaimu Afisa Kazi Mfawidhi wa jiji la Mwanza Bw.Gudluck Luginga.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella (watatu kulia) akipeana mikono na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Anselim Peter mara baada ya kufungua mafunzo ya siku tano kwa madaktari na watoa huduma za afya kanda ya Ziwa kuhusu namna ya kufanya tathmini ya ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kwenye ukumbi wa BoT jijini Mwanza Februari 10, 2020.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, akitoa elimu kwa madaktari na watoa huduma za afya wanaoshiriki mafunzo hayo kuhusu namna ya kumfanyia tathmini mfanyakazi aliyepata ulemavu kutokana na kazi.
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, akitoa elimu kwa madaktari na watoa huduma za afya wanaoshiriki mafunzo hayo kuhusu namna ya kumfanyia tathmini mfanyakazi aliyepata ulemavu kutokana na kazi.
 Washiriki wakiwa mafunzoni.
  Washiriki wakiwa mafunzoni.
  Washiriki wakiwa mafunzoni.
  Washiriki wakiwa mafunzoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...