Wajasiriamali wilayani Monduli mkoani Arusha wametakiwa kuboresha vifungashio pamoja na ubora wa bidhaa zao ili ziweze kupata masoko ya ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika Maonyesho ya Ubunifu,Ujasiriamali na viwanda vidogo  yaliyoandaliwa na shirika lisilokua la kiserikali la Okoa New Generation ,Afisa Mipango wa Wilaya ya Monduli Colex Mwakyelu alisema kuwa wajasiriamali wakiboresha bidhaa zao wanaweza kupata masoko ya nje na kuepuka utegemezi wa masoko ya ndani.

Aliwataka wajasiriamali kuboresha vifungashio na kuzitangaza bidhaa zao katika maonyesho makubwa yanayofanyika ili kupata fursa za masoko na kunufaika kiuchumi.

Mkurugenzi wa shirika lisilokua la kiserikali la Okoa new Generation ,Neema Robert amesema kuwa maonyesho hayo yanalenga kuwapatia fursa za kimasoko pamoja na mafunzo ya wajasiriamali ambayo wamekua wakiyatoa katika majukwaa ya vijana yaliyoko katika wilaya hiyo.
Neema aliwataka vijana kutumia fursa zinazowazunguka kubadilisha maisha yao kwa kuwa wathubutu na wabunifu ili waweze kufanikiwa kiuchumi .

"Vijana wanapaswa kujitoa kufanya shughuli za kujitolea na uzalishaji Mali badala ya kusubiri ajira wakati wanaweza kutengeneza fursa kwa kuamua kujitolea kwanza" Alisema Neema

Kwa upande wake Mmoja wa washiriki wa maonyesho hayo Neema Saidi alisema kuwa kupitia maonyesho hayo yamekua fursa ya kupata wateja na kujifunza kupitia wafanyabiashara wengine juu ya ubunifu na uboreshaji wa bidhaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...