Na Woinde Shizza,Arusha 
WAZIRI Wa nishati Dkt. Medard Matogolo Kalemani amewataka wakandarasi Wa ujenzi mradi mkubwa wa kusafirisha umeme wa KV 400 ambao unahusisha ujenzi Wa njia ya umeme na vituo vya kupozea umeme kuongeza kasi kwani mwendo wanaokwenda nao haurizishi.

Amesema mradi huo ambao ulianza kutekelezwa mwezi machi mwaka 2018 na kutakiwa kukamilika na kukabidhiwa Mwezi Mei 31 mwaka huu, mradi huu ulitakiwa use umekamilika kwa asilimia 62 %lakini bado unasuasua kwani kwa sasa umekamilika kwa asilimia 39%kitu ambacho hakirithishi.

Amesema hayo wakati alipotembelea kituo Na kukagua kituo cha umeme Kv400 katika Kijiji cha Lemugur kilichopo wilayani Arumeru mkoani Arusha ambapo alisema kama mradi huu

Unatakiwa kukamilika Mwezi may na imebaki miezi mitatu tu kukabidhi mradi ni vyema waongeze spidi ya ujenzi Hulu akiwataka wakandarasi Wa mradi huo wafanye Kazi usiku na mchana jua na kiangazi ili waweze kumaliza kwa wakati.

"Kwenye swala hili tunataka wakandarasi waongeze spidi ,waongeze vibarua,na wafanye Kazi usiku na mchana ,na kuna jambo nimesikia kuwa kuna baadhi ya vifaa havijafika vipo bandarini ,na vingine avijaja na kwatwakimu ambazo nilizokuwa nazo vifaa vyote vilitakiwa viwe vimefika adi Mwezi February mwaka huu Leo nimesikia taarifa yenu mnasema vipo kwenye shipingi ,sisi hiyo haituhusu wananchi wanataka umeme hawajui mambo ya shipingi ,kaeni na watu Wa bandarini na TRA ili vifaa hivi vitoke mapema na mradi ukamilike hatutaki kusikia tunatarajia kukamilisha Bali tunataka kukabidhiwa mradi" alisema Kalemani

Aidha amelitaka shirika la umeme kuendelea kusimamia mradi huu ili kuwezesha mradi huu kukabidhiwa kwa wakati uliopagwa ,kwani watanzania wanataka umeme kwa haraka ili waweze kuendesha shughili za viwanda nakufikia uchumi Wa kati.

Wakati huo huo amemtaka mkandarasi Wa usambazaji wa umeme wa vijijini REA mkoa wa Arusha nipo kuongeza kasi ya kupeleka umeme katika vijiji 126 alivyopangiwa na kwa wakati ,ambapo alimtaka kuakikisha wanapeleka umeme katika vitongoji vyote vya Lemuguru, Famu ,engukaret viwe vimepelekewa umeme adi ifikapo Mwezi April mwaka huu kuhakikisha amemaliza shughuli zote za usambazaji Wa umeme katika vijiji vyote ambapo alibainisha iwapo atakamilisha ikifika mda huo hatua Kali zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kushitakiwa na kukatwa fedha zake zote .

Aidha amebainisha kuwa kunabaadhi ya wafanyakazi Wa Tanesco wanachafua sura ya shirika ,ambao wanaomba rushwa huku wengine wakiwa natabia ya kuomba wananchi kulipia nguzo jambo ambalo serikali inalipiga marufuku kila siku lakini bado linasikiwa masikioni kwa watu .

" Meneja Wamkoa naomba usikie hakuna kulipia nguzo niseme nikisikia mwananchi kanunua nguzo ,au kulipia mita ama kifaa chochote nitadili na meneja maana nitajua meneja ndio umetuma hivyo simamia kwa makini ,maana wewe ndio nitakuchukulia hatua ikiwemo kukufuta Kazi,simamia hili kwa makini mwananchi anatakiwa kulipia huduma ya umeme makini sio vifaa maana vifaa ni vya tanesco na sio Mali ya wananchi watu "alisema Kalemani.

Kwa upande wake Mratibu na msimamizi wa mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Peter Kigadye alisema SERIKALI imeshawalipa fidia wananchi 4000 waliopisha mradi wa kusafirisha umeme wa msongo mkubwa wa kilovolti 400 kutoka Singida hadi Namanga ambapo zoezi la ulipaji fidia limekamilika vyema na kila mtu amepatiwa stahiki yake.

Amebainisha kuwa 
Mradi huo wa kusafirisha umeme wa kV400 kutoka Singida hadi Namanga utaunganisha nchi za Tanzania na Kenya na unafahamika kama (Kenya – Tanzania Power Interconnector Project), (KTPIP) na pindi utakapo kamilika utasaidia kuongeza ajira kwa wananchi,pia itasaidia kuongeza wawekezaji ,pia mradi huo ukikamilika utasaidia kuongeza pato la Taifa kwani tutaweza kuuza umeme katika nchi zingine.

Amebainisha kuwa watasimamia vyema mradi huo uweze kukamilika kuwa wakati ili mwananchi waweze kupata huduma ya umeme ya uhakika ,na mradi huu ukikamilika utachangia kuongeza na kuchangia upatikanaji Wa umeme kuwa nchi za Afrika mashariki

Akiongea kwa niaba ya Mkuu Wa mkoa Wa Arusha mrisho gambo Mkuu Wa wilaya ya longido Frank Mwaisumbe alisema kuwa mradi huu ndio msingi Wa mambo yote yanayoregemewa katika kufikia uchumi Wa kati Wa Tanzania ya viwanda.
  Waziri Wa nishati Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi Wa lemugur  kilichopo wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Wakandarasi wa ujenzi wa mradi mkubwa Wa kv400 wakimsikiliza waziri Kalemani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...