Na Rahma Khamis Maelezo
Wananchi wametakiwa kujichunguza katika afya yao mara baada wanapojigundua kuwa wanamabadiliko kufika Hospitali ili kupuguza maradhi ya saratani nchini.
Hayo yamelelezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya maradhi ya saratani Zanzibar Dkt Msafiri Marijani katika Ofisi ya Jumuiya ya maradhi yasioambukiza Mpendae wakati wakiadhimisho ya siku ya saratani Duniani.
Amesema maradhi ya saratani ni tishio kwa Dunia nzima kwani inaongoza kwa kuuwa mara moja ukilinganisha na mmaradhi mengine hivyo ni vyema kuchukua tahadhari zaidi ili kupunguza kasi ya maradhi hayo.
Aidha amaefahamisha kuwa saratani iwapo jamii ni uvimbe mpya unaojitokeza katika mwili ambapo chembechembe zake zina nguvu na huenea kwa kasi zaidi hivyo iwapo mtu atabaini athari yeyote kuwahi Hospitali mapema.
Dkt Marijani amefafanua kuwa saratani zinazowapata watu wengi kuwa ni saratani ya matiti, saratani ya mlango wa kizazi na tenzi dume kwa wanaume hivyo jamii iachane na vitishio vinavyopelekea maradhi hayo .
Aidha amesema tatizo linajitokeza kwa jamii kuchelewa kufika Hospitali na wanapokwenda ugonjwa unakua umeshasambaa kwa wingi hivyo ameishauri jamii kufanya mazoezi na kuacha matumizi ya pombe ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.
Nae mwakilishi kutoka Zanzibar Otreach Program Dkt Naufal Kassim amesema kuwa jamii ipatiwe elimu kuhusu maradhi hayo ili waweze kujichunguza wenyewe na iwapo atakua na wasiwasi kuwahi Hospitali mapema.
Kwa upande wa katibu wa Jumuiya ya saratani Zanzibar Zuhura Saleh Amour amesema kuwa wanatoa elimu ya kujichunguza maskulini na kwa sasa wanataka kufika hadi vijijini ili kuwahamasisha na kupunguza kasi ya maradhi hayo .
Siku ya saratani huadhimisha kila ifikapo February 4 ambapo ujumb mwaka huu napambana na nitaendelea kupambana ili kupunguza athari zinazotokana na saratani zanzibar .
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Saratani Zanzibar Dkt.Msafiri Marijani wa tatu (
Kulia) akitoa maelezo kuhusu Ugojwa wa Saratani katika Maadhimisho ya
Siku ya Saratani Duniani hafla iliyofanyika Ofisi ya maradhi
yasioambukiza Mpendae Wilaya ya Mjini.
Muwakilishi kutoka Zanzibar Outreach Program Naufal Kassim wa kwanza
(Kulia) akitoa ufafanuzi juu ya Ugojwa wa Saratani katika Maadhimisho ya
Siku ya Saratani Duniani huko Ofisi ya maradhi yasioambukiza Mpendae .
Katibu wa Jumuiya ya Saratani Zanzibar Zuhura Saleh Amour
akifahamisha kuhusu Ugojwa wa Saratani katika Maadhimisho ya Siku ya
Saratani Duniani hafla iliyofanyika ya maradhi yasioambukiza Mpendae
Wilaya ya Mjini.
Baadhi ya Waandishi wa habari na Wafanyakazi waliohudhuria katika Maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani yaliyofanyika Ofisi ya maradhi yasioambukiza .
Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...