MAHAKAMA ya Mkazi Kisutu imeruhusu kupokelewa kwa hoja za maombi ya mfanyabiashara James Rugemarila ya kutaka asiondolewe katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili yeye na wenzake wawili 

Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon leo Februari 27, 2020 amedai mbele ya hakimu Hakimu Mkazi Mkuu  Huruma Shaidi kuwa kesi hiyo ilikuja kwa kutajwa na upelelezi bado haujakamilika hivyo aliomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hata hivyo, wakili wa utetezi John Chuma anayemwakilisha Rugemarila alidai mahakamani hapo kuwa mteja wake aliwasilisha hoja ya pingamizi la awali ambayo mpaka sasa hawajapata majibu yoyote.

Akijibu hoja hiyo Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amekiri kupokea nyaraka mbili kutoka upande wa utetezi moja ikiwa inamhusu Rugemarila na kudai  kuwa watatoa majibu kwa mdomo mahakamani hapo baada ya upande wa utetezi kuwasilisha hoja zao kwa maandishi na wako tayari kujibu muda wowote ikiwa mahakama itaruhusu.

Aidha Wankyo alitaka kujua kama nyaraka hizo zipo kwenye rekodi ya mahakama ambapo Hakimu Shahid alimueleza kuwa ameziona nyaraka hizo na zipo kwenye rekodi ya mahakama.

Tarehe zilizopita mshtakiwa  Rugemarila alidai mahakamani hapo kuwa aliandika barua kwa kamishna wa TRA kupitia mjumbe wa Takukuru aliyetembelea gerezani akielezea jinsi Benki ya Standard Chartered Hong Kong inavyokwepa kodi huku akieleza kuwa wanaostahili kujumuishwa kwenye kesi ni benki hiyo na si yeye.

Pia  aliandika notisi katika Taasisi tisa ikiwemo Usalama wa Taifa (TISS) akitaka DPP awasilishe hati ya kuachiwa kwake katika kesi hiyo na asipofanya hivyo yeye atawasilisha hoja ya kuiomba mahakama imuondoe katika kesi hiyo.

Kufuatia taarifa hiyo Hakimu Shahid amewaagiza upande wa utetezi kuwasilisha hoja zao kwa maandishi Machi 2, 2020 ambapo upande wa mashtaka walisema watatoa majibu kabla ya Machi 12, 2020 nanuoande wa utetezi utajibu Machi 14, 2020.

Kesi imeahirishwa mpaka Machi 12, 2020 itakapotajwa.

Mbali na Rugemalira washtakiwa wengine ni Habinda Setha mmiliki wa kampuni ya IPTL na wakili Joseph Mwakandege ambapo wote wanakabiliwa na mashitaka 12 yakiwemo ya utakatishaji fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27. Kwa mara ya kwanza Seth na Rugemarila walifikishwa mahakamani hapo Juni 19, 2017.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...