Mkurugenzi wa Idara ya Biashara Vodacom Tanzania Plc, Linda Riwa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni mpya ya “Wajanja hatuzimi data” ambapo wateja wanapata vifurushi na bando zilizoongezwa thamani zaidi pamoja na kifurushi kipya cha data cha JIMWAGE. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Harriet Lwakatare na Mkuu wa Idara ya Bidhaa za wateja Vodacom, Celvin Mmasy. Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika jijini Dar Es Salaam leo. 



Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Vodacom Tanzania Plc, Harriet Lwakatare (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni mpya ya “Wajanja hatuzimi data” ambapo wateja wanapata vifurushi na bando zilizoongezwa thamani zaidi pamoja na kifurushi kipya cha data cha JIMWAGE. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Biashara Vodacom Tanzania Plc, Linda Riwa na Mkuu wa Idara ya Bidhaa za wateja Vodacom, Celvin Mmasy. Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika jijini Dar Es Salaam leo. 
Mkuu wa Idara ya Bidhaa za wateja Vodacom Tanzania , Celvin Mmasy (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni mpya ya “Wajanja hatuzimi data” ambapo wateja wanapata vifurushi na bando zilizoongezwa thamani zaidi pamoja na kifurushi kipya cha data cha JIMWAGE. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Biashara Vodacom Tanzania Plc, Linda Riwa (katikati) na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Vodacom, Harriet Lwakatare . Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika jijini Dar Es Salaam leo.

……………………………………
Menu rahisi, na iliyoko wazi zaidi, Bando mpya ya siku 3 za sauti na data ambazo zinatoa thamani zaidi kwa wateja. 

 Kampuni ya teknolojia ya mawasiliano inayoongoza Tanzania Vodacom Tanzania PLC leo imetangaza kupunguza bidhaa zake katika menu yake kwa asilimia 75 katika jitihada za kuboresha huduma kwa wateja. 

Akiongea wakati wa kutoa tangazo hilo Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa Vodacom Bi Harriet Lwakatare amesema kwamba hatua hii ni mwitikio wa mahitaji ya wateja ambao walipendekeza kuwa menu iliyopita ilikuwa ni ngumu kuifuata kutokana na kuwepo kwa chaguzi nyingi. 

“Tunakusudia kutoa huduma rahisi na zilizoko wazi kwa wateja wetu na menu hii iliyorahishwa inahakikisha kwamba wateja wetu wanaweza kwenda haraka na kwa hatua chache kufikia huduma wanayoihiji” alisema. 

Wateja wa Vodacom wanapata huduma na bidhaa za kampuni kupitia mifumo mbalimbali ikiwemo USSD code ya*149*01#, app ya Vodacom na tovuti ambazo sasa vinatoa chaguzi bora zaidi. 

Kwa upande wake, Bi Linda Riwa, Mkurugenzi wa Idara ya Bishara wa kampuni ya Vodacom amesema “Sisi pia tumesikia kile ambacho wateja wetu wanahitaji. 

Nina furaha kubwa kutangaza kampeni yetu mpya ya ‘Wajanja hatuzimi data” inayowapa wateja wetu unafuu katika matumizi ya intaneti pamoja na uzinduzi wa bando mpya ya Jimwage ambapo wateja wanaweza kupata GB 3 kwa siku 3 kwa shilingi 2,500 tu. Hii inawezesha kila mtu kutumia mtandao wetu Supa kwa bei nafuu na kufaidika zaidi. 

“Pia tumeboresha huduma yetu ya sauti ili kuwezesha wateja wetu kuongea na wapendw wao bila kujali mtandao gani unayoipigia au gharama za ziada kwa mfano huduma yetu ya cheka iliyoboreshwa inatoa dakika 25 kwa shilingi 500 kupigia mitandao yote” 

Akizungumza kuhusu bidhaa za Data, Mkuu wa Idara ya bidhaa za wateja Celvin Mmasy alisema, “uzinduzi wa bidhaa mpya za data zinawezesh kila Mtanzania kuungnishwa kupitia mtandao Supa wa Vodacom yenye uhakika, sidi kubwa kwa bei hafuu”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...