Mtengenezaji wa Juisi katika
Mgahawa wa Henry, Wilayani Bukombe, akijieleza mbele ya Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Zainab
Chaula jinsi wanavyoandaa juisi hizo.

Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akitoa pesa kuwanunulia juice wauzaji wa mgahawa huo.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akikagua usafi kwenye mgahawa huo.

Wauzaji wa mgahawa wakikinga juice waliyonunuliwa na katibu mkuu Dkt. Chaula.
*********************************
Na. Catherine Sungura-Kahama.
Wafanyabiashara wa vyakula na vinywaji nchini wametakiwa kuzingatia usafi wa mazingira wakati wa uandaaji wa bidhaa hizo.
Rai hiyo ilitolewa hivi karibuni
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto – Idara Kuu ya Afya, Dk. Zainab Chaula alipozungumza
wafanyabiashara kwenye Mgahawa wa Henry, Wilaya ya Bukombe, Kijiji cha
Ushirombo, mkoani hapa.
“Mnatakiwa kuzingatia usafi wa
vifaa mnavyotengenezea vyakula pamoja na mazingira yanayowazunguka kwani
bidhaa zenu zinatumiwa na watu wengi wa makundi na rika
mbalimbali,naona mmeweka grasi chini eneo ambalo kwa kulitazama tu si
safi”.Alisisitiza Dkt. Chaula
“Mlipo hapa ni barabarani,kuna
vumbi na hamjafunika vyakula vyenu ni rahisi watu kupata magonjwa ya
mlipuko kama kuhara na kipindupindu endapo yatatokea,hata wajasiriamali
waliopo kwenye maeneo mengine ni vema wakazingatia usafi ili kulinda
afya za walaji, kuwaepusha na magonjwa ya mlipuko”.Alisema.
Naye mtengenezaji wa Juisi katika
Mgahawa huo, Anneth Ngasa alimhaidi Katibu Mkuu huyo kwamba
watahakikisha wanatekeleza yale yote aliyowaagiza kwa mustakabari wa
kuwalinda wateja wao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...