Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dkt. Bashiru Ally akiendelea na ziara yake Mkoani Mtwara kuelekea jimbo la Ndanda kupitia jimbo la Mtama, wazee wameshindwa kuzuia hisia zao kwa Rais Magufuli kwa kuonesha nia ya kutaka kumchangia gharama za fomu za Urais mwaka 2020.

Akieleza kwa niaba ya wazee hao, Mbunge wa jimbo la Mtama Ndg. Nape Mosses Nnaye, ameleeza kuwa wazee wapo tayari na wamejipanga kumchangia gharama za fomu za Urais ili kuonesha mapenzi yao kwake kutokana na namna anavyowajali wazee na wananchi kwa ujumla, hivyo wanasubiri kibali kwa Katibu Mkuu.

Wameyasema hayo asubuhi ya leo  Februari 22, 2020 katika ufunguzi wa shina la Wakereketwa la Kambarage jimboni Mtama.

Katibu Mkuu pamoja na mambo mengine, akifafanua uamuzi huo wa wazee, ameeleza kuwa, nia yao ni njema na imekuwa matamanio ya wazee wengi kufanya hivyo kama wao wa Mtama, amepokea nia yao njema lakini kikubwa wao waendelee kumuombea Mhe. Rais afya njema ili awatumikie zaidi bila kuchoka.

Katibu Mkuu yupo Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, yenye lengo la kuendelea kukirejesha Chama kwa wanachama.
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dkt. Bashiru Ally katika ufunguzi wa shina la Wakereketwa la Kambarage jimboni Mtama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...