Na Felix Mwagara, MOHA, Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amepokea taarifa ya miradi ya maendeleo ya Taasisi za Wizara yake, na kuwataka Watendaji Wakuu wa Taasisi hizo waendelea kuchapa kazi kwa kasi kwa ajili ya maendeleo ya nchi. 

Akizungumza katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo jijini Dodoma, leo, Simbachawene amewataka watendaji hao kuiendeleza miradi mbalimbali iliyopo  sehemu mbalimbali nchini, kwa kufanya kazi kwa kasi na ushirikiano zaidi.
 “Taarifa zenu za miradi nimeisikiliza na pia mnafanya kazi vizuri, lakini lazima muisimamie miradi hiyo kwa kushirikiana kwa umoja wenu ili kufanikisha miradi hiyo iweze kusonga mbele zaidi, “ alisema Simbachawene. 

Taasisi za Wizara hiyo zilizoshiriki kikao hicho ni Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji na Makao Makuu ya Wizara hiyo, ambazo kila Taasisi ziliwasilisha taarifa zake katika kikao hicho, na kujadiliana hatua iliyofikia miradi hiyo, changomoto zilizopo, pamoja na kuzitafutia suluhisho.

Pia kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima, na viongozi hao waliweza kusikiliza miradi hiyo kwa ufasaha na kutoa njia za kuifanikisha zaidi kwa kuiendeleza miradi hiyo.

Baadhi ya miradi iliyowasilishwa katika kikao hicho, upande wa Polisi;, ujenzi wa jengo la Makao Makuu Dodoma, ujenzi wa Kituo cha Polisi Ludewa Mkoani Njombe, ujenzi wa Jengo la Polisi Mkoa wa  Manyara, na upande wa Idara ya Uhamiaji;- ujenzi wa Jengo la Makao Makuu Dodoma, na upande wa Zimamoto;, Ujenzi wa jengo la Makao Makuu Dodoma.

Kwa upande wa miradi ya Magereza; ujenzi wa Gereza Ruangwa Mkoani Lindi, Igunga na Urambo Mahabusu-Tabora, Mradi wa Umwagiliaji Gereza Idete-Morogoro na Gereza Kitengule-Kagera, na Ujenzi wa Kiwanda cha Seremala Msalato-Dodoma, ujenzi wa Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga, na ujenzi wa Kiwanda cha Sukari Gereza Mbigiri-Morogoro. 

Waziri Simbachawene, wiki iliyopita alikabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola, na baada ya makabidhio hayo, aliwataka viongozi wa Wizara hiyo na Taasisi zake, wafanye kazi usiku na mchana ili nchi iweze kusonga mbele. 

Alisema kwasasa Tanzania katika Afrika inaonekana watu wake wanajenga nchi kwa kasi, hivyo heshima hiyo imeletwa na Rais John Magufuli, hivyo Watanzania wanapasawa kuwa mashabiki wake kwa kuunga mkono juhudi hizo yenye nia ya kuiendeleza nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto meza kuu) akizungumza katika kikao cha Watendaji Wakuu wa Wizara na Taasisi zake, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio. Watatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani kailima.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio, akizungumza katika kikao cha Watendaji Wakuu wa Wizara na Taasisi zake, kilichoitishwa na Waziri wa Wizara hiyo, George Simbachawene. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto meza kuu), akimsikiliza Naibu Katibu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima, alipokuwa anazungumza katika kikao cha Watendaji wa Wizara na Taasisi zake kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto meza kuu), akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Uangalizi na Probesheni wa Wizara hiyo, Aloyce Msika, katika kikao cha Watendaji wa Wizara na Taasisi zake kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto meza kuu), akimsikiliza Kamishna wa Urekebu wa Jeshi la Magereza, Tusikile Mwaisabila, alipokua anafafanua jambo baada ya taarifa ya Jeshi lake kusomwa katika kikao cha Watendaji wa Wizara na Taasisi zake kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio (katikati), na Naibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima (kulia), wakifuatilia taarifa za miradi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji iliyokuwa inasomwa katika kikao cha Watendaji wa Wizara na Taasisi zake kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto meza kuu), akimtaka Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mbaraka Semwanza (kulia aliyesimama), kutoa ufafanuzi wa taarifa ya Jeshi lake iliyosomwa katika kikao cha Watendaji wa Wizara na Taasisi zake kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...