Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto)
akimsalimia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima, wakati
alipokuwa anawasili ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam, leo.
Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio waliwasili
katika ofisi hiyo baada ya Katibu Mkuu kuapishwa Ikulu, leo. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio
akiongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima (kulia), wakati
alipokuwa anawasili ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam. Kadio
aliwasili ofisini hapo baada ya kuapishwa Ikulu,jijini humo leo. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio
(kulia) akiwasalimia Watumishi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi wakati
alipokuwa anawatembelea ofisini jijini Dar es Salaam. Kadio aliwasili
ofisi ndogo ya Wizara jijini humo, baada ya kuapishwa Ikulu, leo. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia)
akimsalimia Mtumishi wa Wizara hiyo, Edaline Osima, ofisi ndogo ya
Wizara, jijini Dar es Salaam, leo. Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Christopher Kadio waliwasili katika ofisi hiyo baada ya Katibu
Mkuu huyo kuapishwa Ikulu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akimfafanulia
jambo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio (kushoto), na Naibu
Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima (kulia), katika kikao kilichofanyika
ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam, leo. Simbachawene na Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio waliwasili katika ofisi hiyo
baada ya Katibu Mkuu huyo kuapishwa Ikulu. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio
(kulia), akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima, alipokuwa
anamfafanulia jambo, mara baada ya Katibu Mkuu huyo kuwasili ofisi ndogo
ya Wizara, jijini Dar es Salaam, baada ya kuapishwa Ikulu, leo. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio
(kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Sheria na Hifadhi wa Idara
ya Huduma ya Wakimbizi, Numbilya Mpolo, alipokua akitoa maelezo ya
majukumu yake katika Idara hiyo. Kadio aliwasili ofisi ndogo ya Wizara
hiyo jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuapishwa Ikulu, leo. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (kulia) akiwasalimia Maafisa wa Idara ya Huduma ya Uangalizi na Probesheni wakati alipowatembelea ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam, leo. Kadio aliwasili katika ofisi hizo baada ya kuapishwa Ikulu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...