Na
Amiri kilagalila-Njombe
Jumla
ya meza 100 na viti vimekabidhiwa kwa shule za sekondari wilayani Wanging'ombe mkoani
Njombe ikiwemo shule ya Thomasi Nyimbo,Philipo Mangula, Igwachanya na Wanike huku
kila shule ikipokea meza 25 na viti vyake ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu
ya halmashauri hiyo kuwa na akiba ya meza kwa ajili ya shule zote 16 wilayani
hapo.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi madawati hayo kwa walimu wakuu wa shule hizo, mkuu wa
wilaya ya Wanging'ombe Ally Kasinge
amesema,madawati yametolewa na halmashauri kutokana na mapato ya ndani, lengo
kuhakikisha shule zote za sekondari zinapa madawati ili kukabiliana na
changamoto ya upungufu wa madawati.
“Niwatoe
hofu kwamba utaratibu huu unaendelea,bado ofisi ya mkurugenzi ina deni tena la
kukamilisha agizo hili la mkuu wa wilaya madawati mia mbili,lakini wadau
wengine wa maendeleo wanaendelea kututengenezea madawati,hatimaye kwa mwaka huu
2020 shule zetu zote za za serikali 16 za sekondari zitapata madawati 25 kila
shule”alisema Ally Kasinge
Aidha
Kasinge amesema mpaka sasa kiwango cha kuripoti kwa wanafunzi kidato cha kwanza
kinaridhisha kwa kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wanafunzi wanaotakiwa kujiunga na
kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2020 wameshajiunga na ametoa wito kwa
wazazi ambao bado hawajawapeleka watoto wao shuleni kuwapeleka kabla ya tarehe
14 ya mwezi wa pili mwaka huu.
“Halmashauri
ilikuwa imepangiwa jumla ya watoto 3431 kwa ajili ya kidato cha kwanza kwa
mwaka 2020 na tangu shule za sekondari zifunguliwe tarehe 6 januari 2020 hadi
sasa wanafunzi waliolipoti ni 2987 ambao hawajaripoti ni 444 tu,na hili nalo
nitoe wiki mbili maafisa tarafa simamieni”alisema tena Kasinge
Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya hiyo Anton Mawata amemshukuru mkuu wa wilaya kwa
jitahada za kuhakikisha asilimia 87 ya wanafunzi wameripoti shuleni nakuanza
masomo yao ikiwa ni tofauti na miaka mingine ya nyuma.
“Mwaka
huu hata mwezi haujaisha tumeshafika asilimia 87 kwa kweli inabidi tujipongeze
sana jambo ambalo miaka mingine huwa tunakuta mwezi wa tatu au wanne ndio tunafika
asilimia hiyo kwa kweli inatakiwa tujipongeze sana”alisema Anton Mawata
Baadhi
ya walimu wa shule za sekondari ambao wamepokea madawati akiwemo kaimu mkuu wa
shule ya Igwachanya Amelye Chatanda na shule
ya Philipo Mangula Joseph Gobo wameishukuru serikali kwa kuwakabidhi madawati na kueleza kuwa kupitia
madawati hayo kutasaidia kutatua changamoto ya miundombinu na itachochea ukuaji
wa taaluma.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...