Na.Khadija seif, Michuzi Tv

WAUMINI wa dini zote watakiwa kuliombea Taifa la Tanzania ili kuepuka majanga .

Mtumishi wa mungu Nabii Joshua Aram amesema wakati mwengine taifa linapofikwa na majanga yanayohatarisha maisha ni muhimu waumini wote kuungana na kuwa kitu kimoja ili kuliombea taifa kuepuka majanga na maafa .

"kwa mwaka huu tumeshuhudia majanga ya moto kwenye station ya mafuta kigamboni lakini kwa uwezo wa mungu tumeweza kuliepuka na madhara hayakutokea hivyo basi tuone ni nafasi pekee ambayo mungu ametupa wasaha wakumshukuru na kumuomba amani hata hivyo nchi ya china tumeendelea kushuhudia ugonjwa wa virusi vya corona vikiendelea kuwasumbua tuombe Sana mungu ugonjwa huo usifike nchini kwetu,"

Aidha,Joshua amesema watanzania wanatakiwa kuitumia amani kama tunu ili kujipatia maendeleo. 

"amani haiwezi kudumu pasipo kumuomba mungu aendelee kutujaalia amani hiyo waumini wote tuungane tuombe mungu ili pasitokee mtu,kikundi kitakachoweza kuvuruga amani hii tuliyoachiwa na mababu zetu,"

Hata hivyo amempongeza Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John pombe Magufuli kwa kuendelea kutetea wanyonge na kuhimarisha uchapakazi hasa kwa vijana.

"Magufuli ni Kiongozi wa kipekee anaependa usawa kwa watu wote ndio maana anaitwa rais wa wanyonge hivyo tumuunge mkono na tumuombee pia kwa maana kazi anayofanya sio ndogo hasa linapokuja swala la kuliongoza Taifa,"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...