
Kaimu Katibu Mkuu Idara Kuu ya
Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara Bw. Leornard Mchau akizungumza na
wawakilishi wa msafara wa wa kitaifa wa wa kijinsia wenye lengo la
kutokomeza ukatili wa kijinsia leo jijini Dodoma utakoanzia Mpanda
mkoano Latavi tarehe 24/02/2020.

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya
Nurdin Bilal Shetta akielezea namana watakavyoupamba msafara wa wa
kitaifa wa wa kijinsia wenye lengo la kutokomeza ukatili wa kijinsia
wakati wa mamandalizi ya kuondoka kwa msafara huo leo jijini Dodoma
utakoanzia Mpanda mkani Katavi tarehe 24/02/2020.

Kaimu Katibu Mkuu Idara Kuu ya
Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara Bw. Leornard Mchau akiagana na Msanii
wa Muziki wa kizazi kipya Nurdin Bilal Shetta mara baada ya kuzunumza
na wawakilishi wa msafara wa wa kitaifa wa wa kijinsia wenye lengo la
kutokomeza ukatili wa kijinsia leo jijini Dodoma utakoanzia Mpanda
mkoano Latavi tarehe 24/02/2020.

Kaimu Katibu Mkuu
Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara Bw. Leornard Mchau
(mwenye mvi) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Msafara wa
wa kitaifa wa wa kijinsia wenye lengo la kutokomeza ukatili wa kijinsia
leo jijini Dodoma utakoanzia Mpanda mkoano Latavi tarehe 24/02/2020. Picha Zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
===== ====== =====
Na Mwandishi Wetu Dodoma
Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii imebariki kuanza kwa Msafara wa kitaifa wa wa kijinsia wenye lengo
la kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Akizungumza na
wawakilishi wa Wizara, Wadau kutoka Legal Services Facility, Wildaf na
wasanii wa muziki wa kizazi kipya leo jijini Dodoma Kaimu Katibu Mkuu
Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bw. Leonard Mchau amesema msafara huo
umeandaliwa maalum kupeleka ujumbe wa kupambana na ukatili wa kijinsia
kuelekea maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani.
Bw. Mchau
amewaasa wawakilishi hao wa Msafara huo kupeleka ujumbe huo ambao
utasaidia kuendeleza mapambano ya kutokomeza vitendi vya ukatili nchini
ambavyo vimekuwa vikishamiri kila siku katika jamii.
Ameongeza kuwa
Serikali imeweka mkazo katika kuhakikisha vitendo vya ukatili wa
kijinsia vinatokomea kwa kasi ili watoto na wanawake wanaoathirika na
vitendo hivyo kuoondokana na vitendo hivyo vinavyowanyima baadhi ya haki
zao msingi.
Akizungumza kwa
naiaba ya Wadau Mwakilishi wa Shirika la LSF Bw. Joseph Magazi
ameishukuru Serikali kwa kuwashirikisha waau katika kampeni ya
kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia na wameahidi kuendxelea
kusirikiana na Serikali katika mapambano hayo.
Akizungumza kwa
naiaba ya Wasanii Bw. Nurdil Bilal maarufu kama ‘Shetta’ amesema
watatumia sanaa yao kufikisha ujumbe kwa jamii kwani wao ni mmoja ya
wanajamii na wanapaswa kushirikiana nayo kusaidia kupambana kutokomeza
vitendo vya kikatili katika jamii.
Msafara huu
utaanzia katika mkoa wa Katavi wilaya ya Mpanda tarehe 24/02/2020 na
kuendelea hadi tarehe 05/03/2020 katika vituo vifuatavyo, Sumbawanga,
Rukwa tarehe 25/02/2020 Vwawa, Songwe tarehe 26/02/2020, Mbeya Mjini
tarehe 27/02/2020 Makambako, Njombe tarehe 28/02/2020 Iringa Mjini,
Iringa tarehe 29/02/2020 Tabora Mjini, Tabora Mjini tarehe 01/02/2020
Shinyanga mjini tarehe 03/03/2020 Maswa Simiyu tarehe 04/03/2020.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...