Meneja Mkuu wa Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC Plc.), Bw Michael Bachan (wa pili kulia –waliosimama) akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Bajeti pamoja na maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwenye ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam wakati wajumbe hao walipofanya ziara hivi karibuni ili kufahamu ufanisi wa mfumo wa stempu za kodi za kielektroniki (Electronic Tax Stamp – ETS) unaotumiwa na kampuni hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Bajeti pamoja na maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakimsikiliza Afisa wa Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC Plc.) iliyopo jijini Dar es Salaam, Bw Phibert Fidel (wa tatu kulia) alipokuwa akifafanua kuhusu moja ya bidhaa za sigara zinazozalishwa na kampuni hiyo wakati wajumbe hao walipofanya ziara hivi karibuni ili kufahamu ufanisi wa mfumo wa stempu za kodi za kielektroniki (Electronic Tax Stamp – ETS) unaotumiwa na kampuni hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Bajeti pamoja na maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakimsikiliza Meneja Uzalishaji wa Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC Plc.) iliyopo jijini Dar es Salaam, Bw Godlove Kayanda (kulia) akielezea kuhusu hatua za uzalishaji wa bidhaa za sigara wakati wajumbe hao walipofanya ziara hivi karibuni ili kufahamu ufanisi wa mfumo wa stempu za kodi za kielektroniki (Electronic Tax Stamp – ETS) unaotumiwa na kampuni hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...