Na Said Mwishehe,Michuzi Blogu ya jamii

JUMUIYA ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC)imepitisha bajeti ya fedha ya Dola za Marekani milioni 94,913,815 kwa mwaka 2020/ 2021.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo Dk.Stergomena Tac amesema fedha hizo zitatumika kwenye masuala mbalimbali yanayohusu Jumuiya.

"Pamoja na ajenda mbalimbali ambazo zimejadiliwa ,pia Jumuiya imepitisha bajeti ya fedha kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021. Kikao cha Mawaziri wa SADC kimefanyika kwa mafanikio makubwa kupitia mfumo wa video .Ni mkutano wa kihistoria na tumejadiliana mambo mengi likiwemo la kuendelea kukabiliana na Corona kwa nchi zetu kuwa na mikakati ya pamoja,"amesema .

Alipoulizwa kuhusu kipaumbele cha Jumuiya hiyo  Dk.Stergom amesema kimsingi kuna vipaumbele vinne ambavyo ni kuendeleza ujenzi wa viwanda, Miundombinu, kuendelea kushughulikia ulinzi na usalama na kipaumbele cha nne ni kuendelea kuleta maendeleo ya wananchi wa Jumuiya hiyo.

Awali akizungumzia kikao hicho cha Mawaziri wa SADC ,Dk.Stergomena amesema mkutano huo umefanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa  na kwa kipekee ametoa pongezi kwa Wazirii Mkuu Kassimu Majaliwa kwa  kutenga muda na kuhudhuria mkutano huo wa  historia.

"Nieleze tu kwamba kikao cha mawaziri kimefanyika kwa mafanikio makubwa kwani kupitia video Coference nchi 13 zimeshiriki kikamilifu na nyingine mbili Mawasiliano hayakuwa mazuri. Fedha ambazo zimetumika kununua mtambo wa Mawasiliano ni fedha za sekretarieti ya SADC na wamepata msaada wa TTCL katika kuunganisha Mawasiliano,'amesema.

Hata hivyo amesema ajenda kuu ilikuwa ni kujadili maazimio ya mawaziri wa afya kuhusu kuangalia namna ya kujikinga na virusi vya Corona.

 Hivyo amefafanua kuwa kwa ukanda wa SADC kuna mgonjwa zaidi ya mmoja na umesambaa kwenye nchi mbalimbali,  hivyo wamekubaliana kuwa na mkakati wa pamoja na kila nchi itasimamia mkakati huo.

Pia amesema nchi za SADC zimekuwa zikitumia Bohari ya Dawa (MSD) kufanya manunuzi ya dawa na vifaa Tina, hivyo mawaziri kwenye kikao hicho wamekubaliana MSD ndio itatumika kununua dawa na vifaa tiba kukabiliana na virusi vya ugonjwa huo.

Wakati huo huo amesema Jumuiya hiyo mwaka huu inatimiza miaka 40 tangu kuanzishwa kwake ,hivyo kuna sherehe maalumu ambayo itifanyika kusheherekea miaka hiyo 40 na kwamba Mzee Keneth Kaunda ndio kiongozi pekee iliyobakia kati ya viongozi walioanzisha Jumuiya hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa SADC ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje Profesa Palamagamba Kabudi amesisitiza mkutano huo umefuatiliwa na nchi mbalimbali Duniani kutokana na mfumo uliotumika na kwamba ajenda zilikuwa nane lakini kutokana na uwepo wa tishio la Corona wamekubaliana Juni mwaka huu watakutana tena kumalizia mkutano huo.

Amesisitiza wamekubaliana njia ya video itaendelea kutumika katika kipindi chote cha Corona na kama alivyosema Waziri Mkuu Tanzania imejipanga vizuri kukabilia Corona.
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC jana Jumatano (Machi 18, 2020)  Jijini Dar es Salaam, na baadaye kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu JUMUIYA hiyo kupitisha bajeti ya fedha ya Dola za Marekani  94 913 815 kwa mwaka wa fedha  2020/2021

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...