Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Zena Said(aliyesimama),akizungumza kwenye kikao baina Waziri wa Nishati na wadau mbalimbali wa Mafuta nchini,jijini Dar es Salaam, Machi 17,2020 (Kulia )Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani,( Kushoto) Naibu Katibu Mkuu Mhandisi Leonard Masanja.

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani(wa kwanza kulia) Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati Mhandisi Zena Said(katikati) na Naibu Katibu Mkuu
Mhandisi Leonard Masanja wakiwa pamoja na wadau mbalilimbali wa
mafuta(hawapo pichani) kujadili hatua ambazo nchi itazichukua endapo
uhaba wa mafuta utajitokeza katika kipindi hiki cha Mripuko wa maradhi
ya Virusi vya Corona,jijini Dar es Saalam, Machi 17,2020.

Waziri wa
Nishati, Dkt Medard Kalemani(aliyesimama) akizungumza na wadau wa mafuta
nchini(hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika kwenye ofisi
za Wakala wa Uagizaji Mafuta Kwa Pamoja ( PBPA),jijini Dar es
Salaam,Machi 17,2020,(kulia) Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Nishati na Madini Dustan Kitandula(kushoto) Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Zena Said.

Wadau
mbalimbali wa mafuta nchini wakiwa katika kikao cha pamoja baina ya
Waziri wa Nishati na wadau wa Mafuta nchini, kilichofanyika ofisi za Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja ( PBPA) jijini Dar es Salaam,Machi 17,2020.
………………………………………………………………………………………………….
Hafsa Omar-Dar es Salaam
Waziri wa
Nishati, Dkt.Medard Kalemani, amekutana na kufanya mazungumzo na
wadau wa mafuta nchini kujadili hatua ambazo nchi itazichukua endapo
uhaba wa mafuta utajitokeza katika kipindi hiki cha Mlipuko wa maradhi
ya Virusi vya Corona.
Tukio hilo
lilifanyika Machi 17, 2020 jijini Dar es Salaam, katika ofisi za Wakala
wa Uagizaji Mafuta Kwa Pamoja ( PBPA),na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati Mhandisi Zena Said, Naibu Katibu Mkuu Mhandisi,
Leonard Masanja, Kamishina wa Petroli na Gesi Adam Zuber na viongozi
mbalimbali wa Taaasi za Wizara ya Nishati na wadau mbalimbali wa mafuta
nchini.
Aidha,amesema
kuwa, Serikali imepanga kukutana na wadau hao ili kuona namna bora ya
kuhakikisha mafuta yatapatikana muda wote kulingana na mahitaji ya nchi,
endapo itatokea dharura yoyote kwenye nchi ambazo wafanyabiashara na
wanaponunulia mafuta na kuhakikisha kuwa shughuli zote zinaendelea
nchini .
“ Sisi kama
Serikali pamoja na wadau ni jukumu letu kuhakikisha kwamba mafuta
yanapatikana muda wote tena ya kutosha kuendesha shughuli zenu
wafanyabiashara lakini na kuendesha shughuli za Serikali pamoja na
shughuli za kijamii zote ziendelee kama kawaida”.Alisema
Alisema,nchi
inajenga miradi mingi mikubwa ya kimaendeleo na kiasi kikubwa miradi
hiyo inategemea sana mafuta katika kuendesha shughuli za uendeshaji.
Aliongeza kuwa,
nchi ambazo Tanzania inanunua mafuta, mpaka sasa bado wanaendelea na
uzalishaji wa mafuta na bado hawajafunga mipaka yao,lakini kwa upande
wa Serikali lazima ichukue hatua Madhubuti kwa kushirikiana wadau wake
ili kuweza kujiachia mafuta ya kutosha nchini.
Hata hivyo.Dkt
Kalemani amewatoa wasiwasi watanzania kwamba mafuta yapo ya kutosha ya
hali ya kawaida kabisa ambayo mpaka miezi miwili ijayo yatatosheleza,
mafuta ya dizel,petroli na mafuta ndege yote yanapatikana nchini na
Serikali itajipanga zaidi ili kuwa na mafuta ya siku nyingi zaidi.
Alifafanua
kuwa,hata kama nchi ina mafuta ya kutosha kwa kipindi hiki lakini
Serikali haitakaa kimya na kuona nchi inakosa mafuta ya kutosha kama
Serikali lazima itafute kinga badala ya kusubiri kuhangaika na tiba.
Waziri
Kalemani,aliwashukuru wadau hao wa mafuta kwa michango yao mizuri yenye
uwazi na inayoangalia hali halisi ya upatikanaji wa mafuta inavyoendelea
nchini na kuwapongeza kwa kutoa michango yenye tija ya kulisaidia Taifa
endapo kama itatokea dharura yoyote katika kipindi hiki cha maradhi
Corona.
Nao, wadau wa
mafuta nchini, wameipongeza Serikali kwa kitendo cha kuwaita ili
kuzungumzia suala hilo ambalo limejikita katika kuchukua tahadhari
ambazo zinajitokeza katika kipindi ambacho dharura itayojitokeza na
kuahidi kuwa wapo tayari kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha mafuta
nchini yanapatikana muda wote.
Aidha walitoa
ushauri wa njia mbalimbali ambazo wanaziona zikichukuliwa zitasaidia
katika kukabiliana na uhaba wa mafuta kama hilo tatizo la uhaba
litajitokeza siku za mbeleni.
Njia hizo ni
pamoja na kutafuta wazalishaji wa mafuta wa nchi nyengine endapo wale
wazalishaji wa awali watafunga mipaka ya nchi zao katika kipindi hiko
cha mpito.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...