BENKI Kuu ya Tanzania (BOT) imeeleza azma yake ya kuendelea kuhamasisha taasisi za Umma, wawekezaji binafsi pamoja na kuweka jitihada za kuwawekea mfumo wawekezaji wadogo katika mwitikio wa uwekezaji wa dhamana za Serikali ambao una faida hasa katika kuongeza kipato na kutopoteza Fedha inayowekwa.

Akizungumza leo jijini Arusha katika semina inayotolewa kwa waandishi wa habari za Uchumi na Fedha, Meneja wa Idara ya Masoko na Fedha wa Benki kuu ya Tanzania (BoT), Lameck Kakulu amesema kuwa kuikopesha au kuwekeza kwa serikali kuna faida kwa kuwa kinachowekwa hakipotei.

Amesema kuwa kwa kipindi cha nusu mwaka kuanzia mwezi Juni hadi Desemba 2019 kumekuwa na mwitikio mzuri wa uwekezaji wa dhamana za Serikali ambapo kumekuwa na ongezeko la wawekezaji kwenye minada inayotangazwa kwa zaidi ya asilimia 103 ukilinganisha na kiwango ambacho serikali ilipanga kukopa kwa kipindi cha nusu mwaka.

Aidha amesema kuwa washiriki wakubwa katika minada hiyo ni ni mabenki yanayoshiriki kwa asilimia 67, huku ushiriki mifuko ya pensheni ukipanda kutoka asilimia 8 hadi 20 na ushiriki wawawekezaji binafsi ukipanda kutoka asilimia 2 hadi kufikia asilimia 6.

"Benki kwa kushirikiana na Wizara ya fedha imeendelea kuelimisha na kuhamasisha juu ya uwekezaji huu ambao una faida nyingi ikiwemo mwekezaji kutopoteza Fedha aliyoiweka, riba inahamishika, mwekezaji anaweza kuziuza katika soko la upili na kipato kitolewacho kutoka kwenye dhamana ya Serikali ni kizuri na mwekezaji anaweza kutumia riba kama dhamana katika huduma za kifedha yaani kuzitumia katika kuomba mkopo" Ameeleza Kakulu.

Amesema kuwa Benki kuu na Serikali inahitaji mwitikio zaidi katikauwekezaji kwenye dhamana ya seriakali hivyo elimu ya uhamasishaji na uelewa itaendelea kutolewa zaidi kwa wawekezaji na taasisi za Umma.

Meneja wa Idara ya Masoko ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Lameck Kakulu akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa Habari za Uchumi na Fedha wakati akiwasilisha mada ya “Mwitikio wa wawekezaji kwenye dhamana za Serikali”.
Meneja wa Idara ya Masoko ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Lameck Kakulu akiwasilisha mada ya “Mwitikio wa wawekezaji kwenye dhamana za Serikali” katika semina ya waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali inayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa BoT tawi la Arusha.
Pichani kulia ni Meneja Msaidizi wa Uhusiano na Itifaki BoT, Bi. Vicky Msina akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari za Uchumi na Fedha
Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Ben Mwaipaja akieleza jambo wakati wa Semina ya Waandishi wa Habari za Uchumi na Fedha,inayoendelea jijini Arusha.

Mmoja wa Wanahabari akiuliza swali 
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakifuatilia moja ya mada iliyokuwa ikitolewa na Meneja wa Idara ya Masoko ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Lameck Kakulu wakati akiwasilisha mada ya mwitikio wa wawekezaji kuwekeza kwenye Dhamana za Serikali katika semina hiyo.


Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakifuatilia moja ya mada iliyokuwa ikitolewa na Meneja wa Idara ya Masoko ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Lameck Kakulu wakati akiwasilisha mada ya mwitikio wa wawekezaji kuwekeza kwenye Dhamana za Serikali katika semina hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...