Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mratibu Mkazi wa Shughuli za Umoja wa Mataifa (UN) Bw. Zlatan Milisic Pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw. Antonio Canhandula Jijini Dar es Salaam.
Waziri Kabudi amewaeleza Bw. Milisic na Bw. Canhandula kuwa UN pamoja na UNHCR zimekuwa na mchango mkubwa kwa kuiunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kukuza maendeleo pamoja na zile za kushughulikia masuala ya wakimbizi.
“Kwa ujumla UN imekuwa ikisaidia Tanzania kufanikisha agenda zake za maendeleo endelevu ya kijamii, na kiuchumi hivyo Serikali itaendelea kuhakikisha inaendeleza uhusiano huu," Amesema Prof. Kabudi.
Kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Shughuli za Umoja wa Mataifa nchini (UN) Bw. Milisic amesema kuwa uhusiano wa UN na Serikali ya Tanzania ni wa muda mrefu na hivyo ni jukumu la UN kuhakikisha inaimarisha uhusiano huo na kuuboresha.
“
Ni matumaini yangu kuwa uhusiano huu tutauboresha vizuri na kuimarisha kwa maslahi mapana na maendeleo endelevu ya taifa la Tanzania," Amesema Bw. Milisic Nae Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw. Canhandula amesema wanatambua mchango mkubwa ambao Tanzania imekuwa ikiutoa kuhakikisha inaimarisha ulinzi wa maeneo ya wakimbizi ili wananchi wa maeneo hayo waendelee kuishi kwa amani na utulivu pamoja na kupatiwa mahitaji muhimu kama vile malazi na mavazi.
"Kwa kweli UNHCR tunafurahishwa na jinsi Serikali ya Tanzania ambavyo imekuwa ikipokea wakimbizi na kuwapatia baadhi ya mahitaji muhimu……tunaomba tuendeleze ushirikiano huu kwa maendeleo yetu," Amesema Bw. Canhandula.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba
John Kabudi (Mb) akimfafanulia jambo Mratibu Mkazi wa Shughuli za Umoja
wa Mataifa (UN) Bw. Zlatan Milisic katika Ofisi ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam.
Wizara Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba
John Kabudi (Mb) akiisoma hati ya utambulisho baada ya kuipokea kutoka
kwa Mratibu Mkazi wa Shughuli za Umoja wa Mataifa (UN) Bw. Zlatan
Milisic katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani
(UNHCR) Bw. Antonio Canhandula akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)
kabla ya kukabidhi hati ya utambulisho katika Ofisi ndogo za Wizara
Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba
John Kabudi (Mb) akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi
Duniani (UNHCR) Bw. Antonio Canhandula katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Duniani (UNHCR) Bw. Antonio Canhandula katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...