Watumishi kutoka Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wamepewa mafunzo ya kujikinga dhidi ya virusi vya Corona (COVID-19) pia namna ya kuepuka ugonjwa wa homa ya Ini. Mafunzo hayo yametolewa na Madaktari bingwa wa magonjwa ya mlipuko kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. John C. Rwegasha na Dkt. Lilian Tina Minja katika ukumbi wa mikutano wa BRELA leo tarehe 17/03/2020 jijini Dar es salaam.

Katika mafunzo hayo Dkt. Minja amesisitiza kunawa vizuri mikono kila wakati kwa kutumia sabuni na dawa ya kuua vijidudu kwa angalau sekunde sitini (60), kukaa umbali wa angalau hatua mbili (2) kutoka kwa mtu anaepiga chafya au kukohoa, kuepuka kushika macho, pua na mdomo kwa mikono isiyo safi kwa sababu mikono hushika sehemu nyingi na ni rahisi kubeba vimelea vya maradhi hayo, kuhakikisha kila mmoja na walio karibu yako wanazingatia ustaarabu wa kuzuia pua na mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafya, kubaki nyumbani ikiwa hujisikii vizuri pia kuwasiliana na wataalamu wa afya kupitia namba 0800110124, 0800110125 ili kuongea nao na kukupa maelekezo kwa msaada, vilevile kuepuka sehemu za misongamano  pamoja na kutumia Sanitazer ili kuuwa vijidudu kwenye mikono. 

Aidha Dkt. Rwegasha amewataka wafanyakazi wa BRELA kuwa na utaratibu wa kupima afya ikiwa ni pamoja na homa ya Ini ili kujua afya zao.
Aidha Mtendaji Mkuu wa BRELA amewashukuru Madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Rwegasha na Dkt. Lilian kwa kufika na kutoa elimu ya kujikinga na virusi vya Corona pia kutoa elimu ya homa ya Ini kwa wafanyakazi wa BRELA. Virusi vya Corona (COVID-19) vimedhibishwa kuwepo nchini Tanzania mnamo tarehe 16/03/2020.
 Dr. John. C. Rwegasha akitoa elimu ya kujikinga na homa ya Ini.
 Wafanyakazi wa BRELA wakifatilia kwa umakini mafunzo ya kujikinga na virusi vya Corona COVID-19.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa akifuatilia mafunzo ya kujikinga na virusi vya Corona COVID-19 na homa ya Ini.
 Dkt. Lilian Minja akitoa mafunzo ya Kujikinga na Corona COVID-19  leo 17/03/2020 katika ukumbi wa mikutano BRELA .






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...