Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wajumbe(hawapo
pichani), wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Kumi na Mbili cha Baraza la
Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi ambapo amelitaka jeshi hilo
kuzingatia misingi ya sheria katika kudhibiti viashiria au matendo ya
uhalifu katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika
mwishoni mwa mwaka huu.Ufunguzi wa kikao hicho umefanyika katika Ukumbi
wa Bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Baraza la
Wafanyakazi ambae pia ni Inspekta Jenerali wa Polisi,Simon Sirro
akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Kumi na Mbili cha Baraza la
Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi ambapo ameahidi kupanga bajeti
itakayosaidia kupambana na changamoto mbalimbali kuelekea kipindi cha
Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.Ufunguzi wa
kikao hicho umefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa
Polisi,Oysterbay jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni.

Mwenyekiti wa Baraza la
Wafanyakazi ambae pia ni Inspekta Jenerali wa Polisi,Simon Sirro akitoa
taarifa ya ulinzi na usalama kwa nchi nzima mbele ya Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kulia),muda mfupi kabla ya
naibu waziri kufungua Kikao cha Kumi na Mbili cha Baraza la Wafanyakazi
wa Idara ya Jeshi la Polisi,kilichofanyika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa
wa Polisi,Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akiweka saini katika daftari la wageni
baada ya kuwasili Bwalo la Maafisa wa Polisi,Oysterbay kufungua Kikao
cha Kumi na Mbili cha Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
Serikali
imelitaka Jeshi la Polisi kuzingatia misingi ya sheria katika kudhibiti
viashiria au matendo ya uhalifu katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi
Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Hayo yamesemwa
leo Machi 16,2020 na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi
Hamad Masauni wakati akifungua Kikao cha Kumi na Mbili cha Baraza la
Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi kilichofanyika katika Ukumbi wa
Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
“Napenda
kuwapongeza Jeshi la Polisi chini yako(IGP Sirro),kwa kufanikiwa
kudhibiti matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo dawa za kulevya,ajali za
barabarani na uhalifu mwingine ambao hapo nyuma wote tulishuhudia ukiwa
umeoata mizizi ila napenda kutoa angalizo kuelekea kipindi cha uchaguzi
mkuu mdhibiti viashiria vya uhalifu au matendo ya uhalifu kwa kufuata
misingi ya sheria ili tuweze kupita kwa amani na salama katika kipindi
hicho” alisema Masauni
Akizungumza
katika kikao hicho cha baraza Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambae
pia ni Inspekta Jenerali wa Polisi,Simon Sirro alisema wao kama jeshi
wanaishukuru serikali na wamejipanga kibajeti kuhakikisha wanakabiliana
na changamoto zozote zitakazotokea katika kipindi cha uchaguzi
“Kwa kiasi
tumefanikiwa kutengeneza bajeti itakayochochea usalama wa raia na mali
zao,bajeti iliyoandaliwa itasaidia kutatua changamoto na kwa kuwa kila
uchaguzi una changamoto zake sisi tumejipanga na tunazichukua
chgangamoto kama fursa” alisema IGP Sirro
Watumishi hao wa
Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi wanakutana katika
kikao hicho lengo ni kujadili masuala mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa
bajeti ya mwaka 2019/2020 na Rasimu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi
kwa Mwaka 2020/2021.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...