*Polepole ampa ushauri Mbowe...asema kwenye hili la Corona tuache mzaha kwani madhara yake ni makubwa
Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimetangaza kusitisha mikutano yake ya ndani na hadhara kwa lengo la kuwaepusha wanachama wake na Watanzania kwa ujumla kupata maambukizi ya virusi vya Corona.
Akizungumza leo Machi 17 mwaka 2020,Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Humphrey Polepole amesema Corona ni janga la kidunia na Chama hicho kinaowajibu wa kuwalinda wanachama na Watanzania ili wasiambukizwe Corona, hivyo wameamua kuzuia mikutano ya ndani na ya hadhara.
Amefafanua kuwa Chama kimepokea taarifa ambayo imetolewa na Waziri wa Afya,Manendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ya kuwepo kwa mgonjwa wa Corona na kuongeza kuwa wamepata maelekezo ya Rais Dk.John Magufuli la kutoa maagizo ya mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu usikimbizwe ili kuepuka Corona.
"Uamuzi wa Rais wetu unaonesha hatua za dhati za kuhakikisha nchi yetu watu wake wanakuwa salama ,pia kusitishwa kwa mbio za mwenye na fedha kuelezwa kwenye Wizara ya Afya ili kukabili Corona ukwelo fedha hizo zinakwenda kuongeza bajeti ya Wizara hiyo.CCM tunalojukumu la kuendelea kuwaambia wanachama wetu kuwa tunayo nafasi ya kuchukua tahadhari ya kujiepusha law kufuata maelekezo ya Wizara, Serikali na Watalaam wa afya,"amesema Polepole.
Amefafanua kutokana na maelekezo ya Wizara na Serikali na ndio maana Chama kimeamua kusitisha mikutano yoyote ya kisiasa inayohusu Chama iwe ya vikao vya ndani au mikutano ya hadhara na kwamba wanatambua mikutano ndio afya ya Chama chao lakini wananchi ni muhimu zaidi na hivyo lazima hatua za kuwalinda zichukuliwe.
Pia ameongeza kuwa hata kwa wabunge wa CCM ni vema nao katika kipindi hiki wakasitisha kufanya mikutano ya hadhara kwani kwenye mikusanyiko ya watu ni rahisi watu kuambikizwa Corona.
" Katika.jambo hili la janga la Corona Watanzania wote lazima tusimame pamoja na kumuomba Mungu atunusuru. Tufuate maelekezo ya Serikali , maelekezo ya Chama na maelekezo ya wataalaam,"amesema Polepole na kuongeza tayari Chama kimetoa utaratibu kwenye ofisi zao zote namna nzuri ya akisalimiana ambayo sasa hakuna kushindana mikono wala kukumbatiana.
Pia amesema wametoa utaratibu wa kuhakikisha kwenye ofisi za CCM kunakuwa na dawa ya vimiminika ambavyo vinatumika kuua virusi vya Corona huku akitoa rai kwa taasisi na mashirika mengine nayo kuweka vimiminika hivyo. "Chama kinasisitiza kuwa utaratibu wa kutolewa dawa ya kuua vimelea uendelee kutolewa ili kulinda maisha ya Watanzania. Hata hivyo kuna namna ya kutumia dawa hizo, hivyo ni vema tukaendelea kupata maelekezo ya Wizara na watalaam wa afya.Nasisitiza mikutano ya CCM isimame hadi Serikali itakapotoa maelekezo mengine,"
Alipoulizwa kuhusu kauli ya Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na kufanya mikutano nchi nzima wakati CCM wao wameamua kusitisha,Polepole amejibu kuwa CCM ni Chama kiongozi na hivyo lazima kiwe mfano.Jana asubuhi Rais alitoa maagizo na baadae kidogo Chadema na Mbowe wao wanatangaza mikutano ya hadhara."Hapo ndipo mtajua nani anawapenda Watanzania na nani hawapendi. Corona inaua haraka sana na kibaya zaidi maambukizi yanakuwa makubwa kwenye mikusanyiko ya watu."
Polepole amesema ni vema Watanzania tukaacha mzaha katika janga hilo na kutoa mfano nchi ya China yenyewe imepiga marufuku mkusanyiko lakini nchini kwetu watu wanaendelea na shughuli zao za kutafuta riziki lakini ni wajibu wa kila kiongozi kuhakikisha wananchi hao wanakuwa salama.Hivyo ametoa rai kwa Mbowe na Chama chake kuthamini uhai kwanza.
Ameomba viongozi wa dini zote kuendelea kuomba kwa Mwenyezi Mungu atuepushe na jenga la Corona na kueleza uwepo wa maombi ya viongozi wa dini yamekuwa msaada mkubwa katika nchi yetu kwani kuna majanga mengi Mungu ametunusuru na anaamini hata hili la Corona nalo tutakuwa salama kwa uwezo wake.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole akionesha dawa kimiminika ambayo inatumika kuua virusi vya Corona na kushauri dawa hiyo iweke katika ofisi mbalimbali kwa lengo la kuwalinda wananchi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole akitoa maelekezo ya namna ya kupaka dawa hiyo ambayo ni maalum kuua virusi vya Corona.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...