Charles James, Michuzi TV

WANAUME nchini wametakiwa kutowanyanyasa wanawake kwa kuwadhulumu haki zao, kuheshimu nafasi zao na zaidi kuepuka kuomba rushwa ya namna yoyote pindi wanapohitaji msaada.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi kuelekea kilele cha siku ya Wanawake duniani Machi 8 mwaka huu ambapo kitaifa maadhimisho hayo yatafanyika Mkoani Simiyu.

DC Katambi amesema Wanawake wengi wapewapo fursa hufanya vizuri zaidi na kwa uaminifu kuliko wanaume wengi hivyo kutoa rai kwa wanaume wote wa Jiji la Dodoma na Tanzania kwa ujumla na kwamba ndani ya Wilaya yake hatoruhusu haki ya mwanamke kupotea.

Amesema ndani ya kipindi chake cha uongozi wilaya ya Dodoma amepigania haki za wanawake ambapo amefanikiwa kurejesha haki za wajane 36, Talaka sita, walioporwa nyumba wanne, haki za ardhi 1036, waliokua na changamoto za malezi 12 na wa mirathi wakiwa saba.

" Kwa muktadha huo sisi kama Wilaya ya Dodoma tutaendelea kupambana kuleta usawa ndani ya jamii yetu, haiwezekani suala la mirathi liwe la wanaume tu, au haki ta kumiliki ardhi isiwe ya wanawake, nikiwa DC hapa sitoruhusu hali hiyo.

Sitomvumilia yeyote ambaye atamnyanyasa mwanamke kwa namna yoyote ile, iwe kuomba rushwa ya ngono, kudhulumu haki zao iwe ya ardhi au mirathi. Tutawalinda wanawake ndio Mama zetu," Amesema DC Katambi.

Amesema serikali ya awamu ya tano imeheshimu na kuthamini sana nafasi ya mwanamke katika sekta zote za elimu, ajira, afya, uchumi ikiwa ni pamoja na kuwapa nafasi za kiuongozi, fursa za kupata haki zao za kijinsi, kijamii,  kiuchumi nakulinda usawa na haki za Binadamu na Watoto.

" Rais Magufuli anapaswa kupongezwa kwa namna ambavyo ametoa kipaumbe kikubwa kwa wanawake kwenye serikali yake. Ametoa nafasi kubwa za kiungozi na zenye maamuzi kwa kundi kubwa la wanawake jambo ambalo miaka ya nyuma ilikua ni nadra.

Leo hii Taifa limeweka rekodi ya kuwa na Makamu wa Rais mwanamke, Mawaziri na Manaibu Mawaziri ni wengi kulinganisha na zamani, kwenye u-DC tumeona namna alivyoteua wanawake wengi, hakika ameonesha imani kubwa kwao na tunapaswa kuiga mfano huu," Amesem DC Katambi.

Amesema serikali imekua ikiwalinda wanawake na watoto kwa kutunga Sheria nying zinazolinda na kuheshimu utu na haki zao pamoja na kuridhia na kusaini  mikataba ya Kimataifa yenye kulinda haki ya kijinsi.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi akizungumza kuhusiana na siku ya Wanawake duniani Machi 8 ambapo kitaifa itafanyika mkoani Simiyu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...