Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa ameshiriki kwenye Mkutano wa Jukwaa la kumi (10) la biashara Zanzibar. Lenye kauli mbiu isemayo “Ushirikishwaji katika kuleta maendeleo endelevu kupitia uchumi wa bahari"

Mkutano huo umefunguliwa Leo 07.03.2020 katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar na Mgeni rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa jukwaa la biashara na Rais wa Zanzibar Mhe .Dkt Ali Mohamed Shein ambae amefungua jukwaa hilo ambalo lengo kuu ni kutazama fursa za uchumi wa bluu (Blue Economy) kwa maendeleo ya Zanzibar.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati akilifungua Jukwaa la Kumi la Biashara Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, na kuwashirikisha Wadau wa Sekta Binafsi na za Umma na Wafanyabiashara Zanzibar WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Jukwaa la Kumi la Biashara Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Mhe.Dk. Ali Ali Mohamed Shein


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu. Akizungumza wakati wa mkutano wa kumi wa Jukwaa la Biashara Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
BAADHI wa Wajumbe wa Mkutano wa Jukwaa la Kumi (10) la Biashara Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo pichani) akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Julkwaa la 10 la Biashara Zanzibar , lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...