NAIBU Waziri wa nchi ofisi ya Rais utumishi wa umma na utawala bora.Dkt Mary Mwanjelwa amewataka watumishi House kuweka kipaumbele Kwa watumishi wa umma kuweza kupata nafasi ya kununua nyumba ambazo zinajengwa na taasisi hiyo ya umma.
Amesema licha kutoa kipaumbele Kwa watumishi wa umma lakini pia asilimia nyingine lazima iende Kwa watumishi ambao wapo kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.
Dkt Mwanjelwa ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kutembelea moja ya miradi inayotekelezwa na taasisi ya watumishi house ambazo zimejengwa katika eneo la Gezaulole.kigamboni.
Pia aliwapongeza watumishi house kupitia mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo kuwa wamejitahidi kutegeneza mazingira rafiki Kwa wapangaji huku akiwataka wakandalasi wa nyumba hizo kukamilisha haraka miundombinu ya maji.
"Mmeniambia kwamba machi 28 mwaka huu mtakuwa mmeshakamilisha mradi huu wa maji na watu hawa watapata maji na tarehe hiyo ikifika Kama majin hayatatoka basi mtendaji Mkuu aaza kukata fedha kutokana mkataba."amesema
Ameongeza lazima kila mtu apate kile anachostahili kutokana jasho lake nakwamba kwasababu wanamkataba hivyo wataangalia kiasi gani cha kukata kutokana na kile kilichopo kwenye mkataba.
"Nawaagiza Kama wanashindwa kukamilisha Kwa wakati mradi huu wa maji ambao nimuhimu kuliko umeme .Basi lazima muwakate sehemu ya fedha zao na katika hili mtanipa mrejesho ."amesisitiza Dkt Mwanjelwa.
Pia aliwataka watumishi wa watumishi house kuchapa kazi kwani Serikali hii ni ya Hapa kazi Tu hivyo lazima watu wafanye kazi kweli .
Kwaupande wake mtendaji Mkuu wa Taasisi ya watumishi house Dkt Fred Msemwa alisema wamepokea maelekezo yote ambayo Waziri ametoa na watahakikisha kila kitu kinakamilika Kwa ndani ya muda.
Amesema watahakikisha wanasimamia maeneo ambayo yamebaki ikiwamo ukamilishajii wa mradi huo wa maji Kama alivyoagiza mheshimiwa Waziri.
"Kama alivyoagiza mheshimiwa Waziri sisi Kama watumishi house tutahakikisha tunalisimamia hili la ukamilishaji wa mradi huu mkubwa wa maji na Kama alivyosema akichelewesha mradi kwa maana ukizidi muda tuliokubaliana tutaaza kukata fedha.amesema mtendaji Mkuu Dkt Msemwa 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea mradi wa nyumba zilizopo Gezaulole wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.kulia Mkurugenzi Mtendaji Watumishi Housing Company, Dkt. Fred Msemwa
Mkurugenzi Mtendaji Watumishi Housing Company, Dkt. Fred Msemwa (kulia)akitoa maelezo kuhusu mradi wa nyumba za kampuni hiyo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi ujenzi wa nyumba eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri ,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (wapili kushoto) akikagua nyumba zilizojengwa na Watumishi Housing Company leo eneo la Gezaulole wilaya ya Kigambaoni jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company Dkt. Fred Msemwa.
Naibu Waziri ,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akinawa
mikono kabla ya kuanza kukagua nyumba zilizojengwa na Watumishi Housing Company leo eneo la Gezaulole wilaya ya Kigambaoni jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
mikono kabla ya kuanza kukagua nyumba zilizojengwa na Watumishi Housing Company leo eneo la Gezaulole wilaya ya Kigambaoni jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa(katikati)akitoa ushauri juu ya upangishaji na uuzaji wa nyumba kwa watendaji wa Watumishi Housing Company katika mojawapo ya nyumba alizozikagua eneo la Gezaulole – Kigamboni jijini Dar Es salaam.
Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa barabra katika Mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Gezaulole wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Emmanuel Mssaka wa Michuzi Tv)
Muonekano wa majengo ya Mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Gezaulole wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa Tank la Maji
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...