Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na sekta ya Afya katika nchi za Mashariki mwa Afrika(EANNASO) imesema taarifa zinazohusu upatikanaji wa huduma za afya zimekua hazipatikani kikamilifu na kusababisha hofu kwa watu wenye kuzihitaji.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo,Olive Mumba amesema hayo wakati akizungumza katika kongamano la wadau kutoka Kenya na Tanzania juu ya upatikanaji wa taarifa muhimu wa namna wananchi wanaoishi katika mipaka ya nchi wanachama wa EAC wanaweza kupata huduma hizo.

Amesema nchi sita za EAC zina idadi ya wananchi wasiopungua milioni 177 ambao wanahitaji huduma bora za afya lakini wakati mwingine wamekua wakilazimika kwenda maeneo ya mbali wakati huduma hizo zinapatikana karibu.

“Magonjwa hayana mipaka ya nchi na eneo la EAC lipo kwenye hatari ya magonjwa ya ina mbalimbali yakiwemo ya milipuko, pia tunao watu takribani milioni sita wanaoishi na maambukizi ya VVU ni muhimu wananchi kuwa na taarifa za uhakika sehemu ya kupata huduma,”amesema Mumba

Meneja Programu wa taasisi hiyo,Onesmus Mlewa amesema wamewaleta pamoja wadau wanaoishi katika mpaka wa Kenya na Tanzania wa Namanga ili kuwashirikisha mpango huo na wao kutoa maoni ya namna wangependa kupata taarifa za afya.

“Unakuta kuna mwananchi anayeishi na Virusi vya Ukimwi katika nchi ya Kenya anatumia dawa za kufubaza makali ugonjwa anataka kusafiri kuja Tanzania ni muhimu awe na taarifa atakapofika Dodoma au Morogoro akihitaji dawa atazipata wapi,hizi ni taarifa muhimu kila mtu kuwa nazo,”amesema Mlewa

Amesema wananchi wamekua wakifuata huduma za afya sehemu za mbali wakati zinapatikana maeneo ya jirani jambo hili linasababishwa na kutokua na taarifa sahihi na haitoshi kwa serikali kusema dawa na wataalamu wapo bali taarifa ziwekwe katika njia rahisi ya kila mtu kuzipata.

Naye Mratibu wa mradi huo,Nginael Mariki amesema utekelezaji wa mradi huo utaanzia katika mpaka wa Namanga kisha katika mipaka mingine kwani maeneo ya mipakani kumekua na mwingilino wa kibiashara na kijamii ambao unaweza kueneza magonjwa ya milipuko.

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Eannaso,Olive Mumba akizungumza katika kongamano 
katika kongamano la wadau kutoka Kenya na Tanzania juu ya upatikanaji wa taarifa muhimu wa namna wananchi wanaoishi katika mipaka ya nchi wanachama wa EAC wanaweza kupata huduma hizo lililofanyika jijini Arusha.
Programu Meneja wa Eannaso,Onesmus Mlewa akizungumza namna kanzi data ya taarifa walizokusanya zinavyowasaidia watumiaji ulimwenguni
katika kongamano la wadau kutoka Kenya na Tanzania juu ya upatikanaji wa taarifa muhimu wa namna wananchi wanaoishi katika mipaka ya nchi wanachama wa EAC wanaweza kupata huduma hizo..
Wadau mbalimbali walioshiriki katika kongamano hilo wakifatilia mada kwa umakini
katika kongamano la wadau kutoka Kenya na Tanzania juu ya upatikanaji wa taarifa muhimu wa namna wananchi wanaoishi katika mipaka ya nchi wanachama wa EAC wanaweza kupata huduma hizo..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...