IMEELEZWA kuwa Benki kuu ya Tanzania imeendelea Kuhakikisha inatoa Fedha kuendana na ukuaji wa uchumi nchini, na hiyo ni pamoja na kuangaalia Fedha iliyopo inaendana na kasi ya ukuaji uchumi wa nchi ambao unakua kila mwaka.

Akizungumza wakati wa semina kwa waandishi wa habari kuhusiana na Uchumi na Fedha ,
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Misango amesema kuwa uchumi wa nchi unakua kila mwaka na kwa kipindi cha mwaka 2018 uchumi ulikua kwa asilimia 7 na kwa mwaka 2017 uchumi wa nchi ulikua kwa asilimia 6.8 na kwa kipindi cha  miaka 5 kuanzia mwaka 2014 Hadi 2018 uchumi wa nchi ulikua  kwa asilimia 6.7.

"Uchumi unapokuwa ni kutokana na ongezeko la uzalishaji na kipato, na sehemu ya kipato huchukuliwa na Serikali na hutumika katika shughuli za kimaendeleo ikiwemo kujenga mashule, hospitali na kuboresha miundombinu" Ameeleza.

Amesema kuwa benki kuu inatoa Fedha kwenda kwenye uchumi kwa njia mbili ikiwemo kwa Serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kiuchumi na fedha kuzunguka kwa namna mbalimbali na pia benki kuu hutoa fedha na kushirikiana kwa karibu na mabenki mbalimbali.

Ameeleza kuwa mabenki mengi yamekuwa yakitoa mikopo kwa taasisi binafsi kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi hali inayopelekea mzunguko wa fedha kuwa mkubwa.

"Wananchi lazima waelewe kwa sasa mzunguko wa fedha unaenda kwa haraka na hiyo ni kutokana na mifumo mbalimbali ya malipo" amesema.

Kuhusiana na mwenendo wa biashara hasa kwa wafanyabiashara wadogo ameeleza kuwa fedha ni nyingi na bidhaa na huduma ni chache katika uchumi hali inayopelekea mfumuko mkubwa wa bei.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...