Sehemu
ya waandishi wa habari za mazingira kutoka vyombo mbalimbali nchini wakiwa
kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za
Mazingira(JET) hivi karibuni jijini Dar
es Salaam kwa lengo la kuwajengea uwezo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa JET John Chikomo(kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya JET Dk.Ellen
Utaru Okoedion wakijadilana jambo wakati
wa mafunzo hayo.
:Mwandishi
Sidi Mgumia akitoa uzoefu wake katika masuala ya uandishi wa habari za
mazingira na uhifadhi wakati wa semina hiyo iliyoandaliwa na JET hivi karibuni
jijini Dar es Salaam.
:Baadhi
ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa katika semina ya waandishi wa habari za
mazingira iliyofanyika hivi karibuni.
Mhariri
mkongwe Jackton Manyerere(kulia) na Mwandishi Mwandamizi wa gazeti la Nipashe
Salome Kitomari(kushoto)wakifuatilia kwa mafunzo yaliyohusu namna ya kuandika
habari za mazingira na uhifadhi.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya JET Ellen Utaru Okoedion (aliyesimama) akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari za mazingira
Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Mazingira
Tanzania(JET) moja uya mkakati wake ni kuhakikisha inaendelea kuwajengea uwezo
waandishi wa habari nchini kuwa na uelewa mpana wa kuandika habari za mazingira
na uhifadhi.
JET wamekuwa na utamaduni wa kuandaa mafunzo kwa
waandishi wa habari na hasa waliojikita kwenye kuandika habari zinazohusu
mazingira nchini. Kwa sehemu kubwa mafunzo hayo yamekuwa chachu kubwa ya
kuifanya jamii nayo kupata habari sahihi zinazohusu mazingira kupitia waandishi
ambao wamepita kwenye mikono ya JET.
Kwa kutumia watalaamu wa masuala ya mazigira na
uhifadhi kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania wamekuwa daraja na kiunganishi
muhimu katika ya wadau wa mazingira wakiwemo waandishi wa habari.
Mbali ya JET kutoa mafunzo yanayohusu mazingira na
uhifadhi imekuwa na uratibu wa kuandaa ziara katika maeneo mbalimbali ya
uhifadhi nchini na hivyo kutoa fursa kwa waandishi kujifunza kwa vitendo.
JET wamekuwa wakifanikisha mafunzo na ziara hiyo
kupitia ushirikiano uliopo kati yao na
na USAID-Protect ambao wamekuwa wadau wakubwa na wa muda mrefu katika
kuhakikusha mazingira na uhifadhi nchini Tanzania unakuwa salama.
Kwa kukumbusha tu JET imekuwa na mtandao mpana wa
waandishi wa habari ambao ni sehemu ya wanachama wao na kwa sehemu kubwa
wamejikita kuandika habari zinazohusu mazingira .
Hivyo kwa JET kwa kutambua umuhimu wa uhifadhi wa mazingira
nayo imeamua kubeba jukumu la kuhakikisha inatumia kila aina ya chombo cha
habari kuhakikisha umma wa Watanzania unakuwa na taarifa sahihi zinazohusu eeo
hilo. Hakika JET wamefanikiwa na wanastahili pongezi kutokana na kubeba jukumu
hilo kwa maendeleo ya Taifa letu.
Katika muendelezo huo wa utoaji wa mafunzo, siku za
hivi karibuni JET iliandaa mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari za mazingira
ambapo mada mbalimbali zilitolewa kupitia watalaamu waliobobea kwenye sekta ya
mazingira na uhifadhi.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika hivi
karibuni jijini Dar es Salaam,
Mwenyekiti wa JET, Dk. Ellen Otaru ametumia nafasi hiyo kufafanua Chama hicho
kimejitahidi kuboresha ufikishwaji wa taarifa kwa mwananchi ili mtanzania
aelewe kuhusu mazingira anayoishi na jinsi ya kuishi nayo bila kuleta
uharibifu.
"Yote tunayoyafanya tunamuelisha Mtanzania kwa
ujumla wake ili afahamu kwa kina nini maana ya mazingira, nafasi yake kwenye
hayo mazingira na yale mazingira yana umuhimu gani kwa faida yake na nchi yetu
kwa ujumla,"amesema na kuongeza ili kuifikisha elimu hiyo kwa usahihi
lazima wanayoipeleka nao wawe wameelimishwa vya kutosha
Dk.Otaru amesema
JET imekuwa mdau mkubwa katika
kupanga mikakati ya sera na sheria katika kuangalia inafanya vipi
kuhakikisha inafanikiwa na kama zinakwenda sambamba na mahitaji yote hayo
yanatokana na kalamu za wanahabari na nini kikifanyika jamii itaweza kushiriki
kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira.
Hata hivyo amesema JET inafanya yote hayo kama sehemu
ya lengo la kundeleza kizazi hadi kizazi ili kiweze kupata yale ambayo wao
wameyarithi kutoka vizazi vilivyopita na kwa kufanya hivyo kutasaidia jamii
kuwa na uelewa na hatimaye kuyatunza mazingira ili nayo yawatunze.
"Ni wajibu wa kila mmoja wetu kufukiria nini
kifanyike ili tuendeleze nchi yetu kwa kuangalia mfumo mzima wa wanyamapori,
binadamu pamoja na uchumi ambao wengi tunategemea kupitia
wanyamapori," amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Nukta Afrika,
Nuzulack Dausen akizungumza wakati wa mafunzo hayo amewahimiza waandishi wa habari kufanya habari za
uchunguzi zinazohusu wanyamapori na mazingira kwa lengo la kuelemisha jamii na
kulinda hifadhi zilizopo kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Pia amewashauri waandishi wa habari kutumia kifaa cha
kielektriniki kisicho na rubani (Drone) kwa ajili ya kufanya habari za
uchunguzi kwenye maeneo ya hifadhi na mbuga za hapa nchini ili kubaini
majangili wanaoingia katika hifadhi hizo.
"Ili mwandishi aweze kufanya habari yake vizuri
ni lazima atengeneze 'network' na wakati anatengeneza lazima ajue uhusiano na
watoa taarifa wake ili aweze kufanya kazi yake kwa njia rahisi na kujua nani ni
nani na anafanya nini,"amesema.
Pia, amesema pindi mwandishi wa habari anapokwenda
kufanya mahojiano anatakiwa kuuliza maswali mengi ili kupata mambo mengi
ikiwemo kujua ulewa wa watu ambao anawafanyia mahojiano na hiyo itamsaidia
kufahamu vitu vingi kwa wakati mmoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...