MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imesema kutokana ugonjwa wa Corona kuendelea kuwa tishio duniani na hata kama ikitokea Mahakama zikatakiwa kufungwa basi shughuli za kimahakama hazitasimama na badala yake zitakuwa zikifanyika kwa njia ya mtandao.
Pia imeelezwa kuwa kuanzia kesho mahabusu ambao walikuwa wanapaswa kuletwa Mahakama Kuu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kusikiliza kesi zao hawataletwa, badala yake utatumika mfumo wa vedio maarufu video comference kwa ajili ya kuendesha kesi hizo.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania, Ezekiel Felshi wakati akuzungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kwamba mfumo huo wa video Conference utakuwa ukianza saa saba mchana Mahakama Kuu ili kupisha asubuhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufanya hivyo.
"Watuhumiwa wapelekwe mahakamani baada ya upelelezi kukamilika," amesema Jaji Felshi.
Wakati Mahakama Kuu ikitoa maelezo hayo kama sehemu ya kukabiliana na tishio la uwepo wa virusi vya Corona nchini, tayari Serikali kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wameshatoa maelekezo ya nini ambacho kinatakiwa kufanyika katika kipindi hiki kuepuka kuenea kwa ugonjwa huo.
Pia Serikali imetoa malekezo mbalimbali yakiwemo ya kuepukwa kwa mikusanyiko isiyokuwa ya lazima, mikutano, washara na makongamano huku Watanzania wakitakiwa kuchukua tahadhari kwa kunawa mikono mara kwa mara lakini hakuna sababu ya kutishana kuhusu ugonjwa huo na kubwa zaidi watu waendelee kuchapa kazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...