Jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Arusha likiwa katika hatua za
awali za ujenzi wake ulioanza Januari 2020. Jengo hili na mengine sita
ni majengo yanayojulikana kama Vituo Jumuishi vya utoaji haki yaani
yatakayokuwa yakitoa huduma za Mahakama ngazi zote katika jengo moja.
Majengo haya yanajengwa katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma, Morogoro
na Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Majengo wa Mahakama ya Tanzania Mhandishi Khamadu Kitunzi akiwaelezea jambo wajumbe wa Kamati wa Mahakama ya Tanzania a kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wakikagua jengo jipya la Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara.
Na Lydia Churi-Mahakama, Arusha
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imeanza ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa baadhi ya majengo ya Mahakama ya Tanzania ambapo imeridhishwa na miradi ya Kondoa, Manyara na kituo Jumuishi cha utoaji Haki kilichoanza kujengwa mkoani Arusha.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini Mhe. Emmanuel Mwakasaka ameipongeza Serikali kwa hatua iliyofikiwa ya ukamilishwaji wa ujenzi wa majengo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara, Mahakama ya Wilaya ya Kondoa na kuanza kwa ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu Arusha ambalo litakuwa likitoa huduma kama kituo Jumuishi cha utoaji haki.
Mahakama ya Tanzania imeanza ujenzi wa majengo sita yenye gorofa 3 kila moja katika mikoa mitano nchini ambayo ni Arusha, Mwanza, Dodoma, Morogoro na Dar es salaam yanayotarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi kumi ijayo. Majengo hayo ya Mahakama Kuu yanayojulikana kama vituo Jumuishi vya utoaji haki yatakuwa na ngazi zote Mahakama (Mahakama za Mwanzo mpaka Mahakama Kuu) pamoja na ofisi za wadau kwa lengo la kurahisisha huduma za utoaji haki.
“Miradi ya ujenzi wa majengo ya Mahakama imeenda kwa haraka sana, hatukutegemea hili, tumeridhishwa sana na kazi iliyofanyika, pongezi kwa watendaji wote wa Mahakama”, alisema Mhe. Mwakasaka.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara, waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa kutekeleza miradi ya ujenzi wa majengo ya Mahakama katika maeneo mbalimbali nchini.
“Kwa hali tuliyoikuta leo inaonesha kuna kazi kubwa imefanyika na muonekano wa jengo sasa ni mzuri, limekamilika,alisema waziri huyo.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imeanza ziara ya kikazi ambapo wajumbe wake wamekagua miradi ya ujenzi wa majengo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara na Mahakama za wilaya za Kondoa na Longido pamoja na ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu kanda ya Arusha.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...