Baadhi ya wakazi
wa kijiji cha Nyange, wilayani Kilombero, wakitoa vifaa vyao kwenye
makazi yao yaliyozingirwa na maji kutokana na athari ya maafa ya
mafuriko. Jumla ya Kaya 250 zilizokuwa zimezingirwa na maji zimeokolewa
na kuhifadhiwa shule ya sekondari Nyange.
Kufuatia Kaya 250
katika kata ya Msolwa Stesheni katika kijiji cha Nyange Wilayani
Kilombero kuathirika na athari za maafa ya mafuriko. Kamati ya
Usimamizi wa Maafa ya Wilaya hiyo imeelekezwa kufanya tathmini ya awali
kwa kata ya Mbanane na Kichangani ambazo takribani watu 350
wameathirika na maafa hayo yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea
kunyesha hapa nchini.

Mkuu wa Wilaya ya
Kilombero, Mhe. James Ihunyo, akimhakikishia Mkurugenzi Idara ya
Menejimenti ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe
kufuatilia Kamati ya maafa kufanya tathmini ya awali ya athari za maafa
katika kijiji cha Nyange Wilayani Kilombero wakati Mkurugenzi huo
alipokutana na kamati hiyo, Machi, 2020.


Mkurugenzi Idara
ya Menejimenti ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe
akimueleza Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. James Ihunyo, umuhimu wa
Kamati ya maafa kufanya tathmini ya awali ya athari za maafa katika
kijiji cha Nyange Wilayani Kilombero wakati Mkurugenzi huo alipokutana
na kamati hiyo, Machi, 2020.

Mkurugenzi Idara
ya Menejimenti ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe
akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. James Ihunyo, mablanketi
kwa ajili ya waathirika wa mafuriko wa Kijiji cha Nyange waliohifadhiwa
katika shule ya sekondari Nyange, wilayani Kilombero, Machi, 2020.

Mkurugenzi Idara
ya Menejimenti ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe
akiongea na baadhi ya waathirika wa mafuriko wa Kijiji cha Nyange
waliohifadhiwa katika shule ya sekondari Nyange, wilayani Kilombero,
Machi, 2020.

Mkuu wa Wilaya ya
Kilombero, Mhe. James Ihunyo, akiongea na baadhi ya waathirika wa
mafuriko wa Kijiji cha Nyange waliohifadhiwa katika shule ya Sekondari
Nyange, wilayani Kilombero, Machi, 2020.

Baadhi ya vifaa
vya nyumbani vya wakazi wa Kijiji cha Nyange vikiwa vimehifadhiwa kwenye
shule ya sekondari Nyange, baada ya kijiji hicho kupata atthari ya
maafa ya mafuriko, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo
mbalimbali hapa nchini.
*****************************
Kufuatia Kaya 250
katika kata ya Msolwa Stesheni katika kijiji cha Nyange Wilayani
Kilombero kuathirika na athari za maafa ya mafuriko. Kamati ya
Usimamizi wa Maafa ya Wilaya hiyo imeelekezwa kufanya tathmini ya awali
kwa kata ya Mbanane na Kichangani ambazo takribani watu 350
wameathirika na maafa hayo yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea
kunyesha hapa nchini.
Akiongea mara
baada ya kukagua athari za maafa katika kata hizo, wilayani Kilombero,
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali
Jimmy Matamwe, amesema tathmini ya awali ya athari za maafa katika kata
hizo hainabudi kufanyika kwa haraka ili kubaini hatua za kuchukua katika
kukabiliana na maafa hayo.
“Kwa mujibu wa
Sheria ya Usimamizi wa maafa Na. 7 ya mwaka 2015, inaainisha majukumu
ya kamati za usimamizi wa Maafa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi mkoa,
ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, jukumu la msingi ni kutafuta
rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika ngazi husika, pamoja
na Kuratibu na kusimamia shughuli za usimamizi wa maafa na operesheni
za dharura ndani ya Kijiji wilaya au mkoa. Hivyo kamati hii haina budi
kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.”amesisitiza Kanali
Matamwe.
Awali akieeleza
hatua ambazo kamati ya Menejimenti Usimamizi wa Maafa ya Wilaya hiyo
ilizo zichukua, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. James Ihunyo,
amefafanua kuwa hadi kufikia tarehe 20 Machi 2020, kamati hiyo ilikuwa
imefanikiwa kuwaokoa watu 350 ambao wamehifadhiwa kwenye shule ya
sekondari Nyange.
“Tunaishukuru
serikali kupitia, Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya uratibu wa shughuli za
maafa kwa miongozo, lakini pia na kufika kwa wakati katika kata zetu,
tumefurahi na mmetuletea mablanketi ambayo naamini yatawasaidia
waathirika wa maafa haya ambao tumewahifadhi hapa shuleni. Kwa sasa wapo
wanaume 172 na wanawake 178 huku watoto ni 30 ambao tumewahifadhi”
Ameeleza Mhe. Ihunyo.
Kwa mujibu wa
Taarifa ya Mamlaka ya Hali hewa iliyotolewa mwezi Februari mwaka huu
imeeleza kuwa kutakuwa na mvua za juu ya wastani katika eneo kubwa la
nchi kati ya mwezi Machi hadi mwezi Mei, mwak huu, ambapo mvu ahizo
zilitarajiwa kuanza kati ya wiki ya kwanza au ya pili ya mwezi Machi na
kutaraji akumaliziaka kati ya wiki ya kwanza au ya pili yamwezi Mei.
Hivyo kutokana na mvua hizo wananchi hawanbudi kuchukua tahadhari za
athari za mvua hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...