Waziri wa afya wa Kenya Mutahi Kagwe ametangaza kuwa watu wengine wanane wamethibitishwa kuwa na ugonjwa wa corona nchini humo. Ongezeko hilo linafikisha 15 idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo hatari.
Walioambukizwa ni Wakenya watano na raia watatu wa kigeni walio na umri wa kati ya miaka 20 hadi 57.
Wanane hao waliingia nchini kupitia uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta kati ya Machi 4 na 17.
Serikali kwa sasa inafanya juhudi ya kuwatafuta waliotangamana nao ili kudhibiti maambukizi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...