Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki BaloziCol. Wilbert A. Ibuge katikati akimkaribisha Balozi wa Vietnam chini Mhe.Nguyen Kim Doanh katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma alipofika kuitikia wito wa Katibu Mkuu kulia ni KaimuMkurugenzi anayeshughulikianchi za Asia na AustralasiaBw. Ceasar Waitara.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki BaloziCol. Wilbert A. Ibuge (kulia) akizungumza na Balozi wa Vietnam chini Mhe.Nguyen Kim Doanh katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma alipofika kuitikia wito wa Katibu Mkuu

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki BaloziCol. Wilbert A. Ibuge (kulia) akizungumza na Balozi wa Vietnam chini Mhe.Nguyen Kim Doanh katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma alipofika kuitikia wito wa Katibu Mkuu
Balozi wa Vietnam chini Mhe. Nguyen KimDoanh (katikati) akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki BaloziCol. Wilbert A. Ibuge (kulia) alipofika katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma kuitikia wito wa Katibu Mkuukushoto ni afisa ubalozi wa Vietnam aliyefuatana na Mhe. Balozi Nguyen.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Wilbert Ibuge na Balozi Nguyen Doanh waVietnam wakiangalia nyaraka mbalimbali walipokutana Ofisini jijini Dodomakuzungumzia namna ya kuimarisha na kuboresha mahusiano ya kihistoria yaliyopo
baina ya Tazania na Vietnam.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Wilbert Ibuge na Balozi Nguyen Doanh waVietnam wakiagana walipomaliza mazungumzo yao Ofisini jijini Dodoma .

KatibuMkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki BaloziCol. Wilbert A. Ibuge leo tarehe 26 Machi, 2020 amekutana na kufanya mazungumzona Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Kim Doanh katika ofisi za Wizara,Makao Makuu, Jijini Dodoma.

BaloziDoanh alikuja jijini Dodoma kufuatia wito wa Balozi Ibuge na kufanya mazungumzo yaliyohusu mambo mbalimbali kuhusu mahusiano baina ya Tanzania na Vietnam, likiwemosuala la uwekezaji wa Vietnam nchini kupitia Kampuni ya simu ya Halotel.

Katikamazungumzo yao, viongozi hao wamekubaliana kuendelea kuimarisha mahusianobaina ya Nchi mbili hizo, ikiwemo uendelevu wa mawasiliano ya Kidiplomasiaambapo mahusiano ya Tanzania na Vietnam yamefikisha miaka 55 mwaka huu huku fursa za uwekezaji nchini zikiendeleakuimarishwa na hivyo kuiwezesha Serikali ya Vietnam ambayo ni mmiliki waKampuni ya Simu ya mkononi ya Halotel kuwekeza nchini na kuendesha shughuli zake.

Balozi Ibugepia alimjulisha Mhe. Balozi Doanh kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Wizaraitaendelea kuhimiza uwekezaji kutoka Vietnam na kusisitiza uwekezaji huokuzingatia sheria za nchi, kwa lengo la kuwepo tija kwa pande zotezinazohusika.

Kufuatiakikao hicho, Mhe. Balozi Doanh aliahidi kuendelea kuyasisitiza makampuni yaVietnam Nchini ikiwemo kampuni ya Halotel kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanunizilizowekwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuhakikisha
pande zote mbili zinanufaika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...