Charles James, Michuzi TV

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Queen Mlozi amempongeza Rais Dk John Magufuli kwa kuwapa nafasi za uongozi wanawake kwenye serikali yake ya awamu ya tano.

Katibu huyo ametoa pongezi hizo pamoja na kumuomba Rais Magufuli kuendelea kuwapa nafasi kwani waliopo wameonesha jinsi gani mwanamke akipewa nafasi anaweza kufanya vizuri.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani itakayofanyika Machi 8, Queen amesema awamu ya tano chini ya Rais Magufuli imeweka rekodi ya kutoa kipaumbele kwa wanawake katika nafasi mbalimbali.

" Hakika awamu ya tano imeweka rekodi ya kuwa na viongozi wengi wanawake na wamefanya vizuri sana, kuanzia kwa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Naibu Spika, Mawaziri na viongozi wengine wote wamefanya kazi zao kwa weledi mkubwa sana.

Ninaomba Mhe Rais aendelee kuwapa nafasi kwani mwanamke akipewa nafasi anaweza kufanya vizuri na kwa uadilifu mkubwa, kama wanawake tunamshukuru Rais Kwa kutuamini na kutupa nafasi ya kumsaidia kwenye serikali yake," Amesema Queen.

Kuhusu Uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika Oktoba mwaka huu, Queen amesema hakuna shaka kwamba Rais Magufuli atashinda Kwa kishindo kikubwa kwani amefanya mambo mengi ya kimaendeleo ambayo yalikua kama ndoto Kwa watanzania hapo awali.

Amesema miradi ya kimkakati inayoendelea Nchi nzima, elimu bure pamoja na wingi wa vituo vya afya ni mambo ambayo yalikua mtambuka miaka ya nyuma lakini chini ya Rais Magufuli kila kitu kimewezekana.

" Kwa kweli sisi wanawake tunamuunga mkono sana na ana kura zetu za kutosha. Hii miaka mitano amefanya mambo makubwa mno. Ahsante pekee kwake inayomstahili ni kura ya ndio kwenye uchaguzi mkuu.

Lakini pia niwaase wanawake nchini kujitokeza Kwa wingi kuwania nafasi za Ubunge na udiwani katika uchaguzi ujao, wasiogope uwezo tunao na nafasi tunayo tujitokeze Kwa wingi," Amesema Queen.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Queen Mlozi akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma kuelekea siku ya wanawake Machi 8 ambayo kitaifa itafanyika mkoani Simiyu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...