Viingilio vya mchezo wa raundi ya pili ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga vyawekwa hadharani.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limetangaza viingilio ni shiling 7000
kwa viti vya mzunguko, Viti vya Machungwa vikikaliwa kwa shilling 1000,
VIP B na C itakuwa ni 15000 na VIP A kwa shiliing 30,000.
Taarifa
hiyo iliyotolewa na TFF mapema leo, imeeleza kuwa mchezo huo utapigwa
majira ya sa 11 jioni katiia Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Mechi
hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa pande zote, itachezwa siku
ya Jumapili ya Machi 08, huku kila upande ukijinasibu kuibuka kidedea.
Ikumbukwe
kuwa katika mchezo wa kwanza uliochezwa January 04, Timu hizo zilitoka
sare ya goli 2-2 Simba wakitangulia kufunga magoli yaliyofungwa na
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Rwanda Meddie Kagere na Deo Kanda ambapo
Yanga walisawazisha kupitia kwa Kiungo Mapinduzi Balama na Mohamed Issa
'Banka'.
Simba kwa sasa
wanaongoza msimamo wa ligi Kuu wakiwa na alama 65 na siku ya Jumatano
atashuka dimbani kuvaana na vijana wa Chamazi Azam Fc katika mchezo wa
Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga
nao wapo nafasi ya nne wakiwa na alama 45, watacheza kesho dhidi ya
Mbao Fc ya Jijini Mwanza ambapo michezo yote hiyo itapigwa majira ya sa 1
usiku.
Tambo za mashabiki wa pande zote mbili zinaendelea kila mmoja akiamini anaenda kuondoka na alama tatu muhimu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...