NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
NAIBU
Katibu Mkuu Taifa,CCM Rodrick Mpogolo ,amewapa salamu wapinzani wa
ndani ya Chama ama wa Vyama vingine vya upinzani wamuache Rais dk.John
Magufuli afanye kazi na amewashangaa wanaojaribu kupimana nae ubavu
,wajue wamechemsha.
Pamoja
na hilo ,ameeleza mabalozi wa chama ndio mpango mzima na mashina ndio
nguvu ya chama hivyo kuna kila sababu ya kuwaheshimu na kuwathamini
mabalozi hao katika utekelezaji wa majukumu yao.
Akizungumza
katika mkutano mkuu wa Jimbo la Kibaha Mjini, mkutano ambao mbunge
Silvestry Koka alipata wasaa wa kueleza utekelezaji wa ilani ,Mpogolo
alisema Rais ni mtu wa vitendo, anatekeleza na zipo nchi zinatamani
utendaji kazi wake hivyo tuendelee kumuamini .
Alieleza
,mwenyekiti wa CCM Taifa anatekeleza mambo makubwa ya kiuchumi na
kimaendeleo kwa maslahi ya watanzania,sasa akitokea ambae haoni
yanayofanywa atakuwa ana shida.
"Wapo
baadhi ya watu wakipata madaraka wanasahau kuheshimu wenzao,na wengine
wakiomba kura wakipata wanajisahau wale waliowapa kura"CCM ni
kuheshimiana kiongozi anapaswa kumheshimu mwanachama na mwanachama
amuheshimu kiongozi"nina wakumbusha alisema Mpogolo.
Katika
hatua nyingine, alisema chama kinaendelea kuwajibisha wale wanaokiuka
kanuni na taratibu na bado kipo imara na hakijatikisika.
Hata
hivyo,naibu katibu mkuu huyo alisema nguvu ya mamba ipo kwenye maji na
nguvu ya CCM ipo kwenye mashina hivyo hatuwezi kushinda vita ya uchaguzi
kama tutawatenga mabalozi.
"Viongozi
wote kuanzia mkoa,wilaya ,kata wote tupo chini ya mabalozi, hawa
mabalozi ndio tunapaswa kuwaheshimu ,wao ndio nguvu ya chama na ndio
ushindi wetu":alisisitiza Mpogolo.
Mpogolo
alimpongeza Koka kwa utekelezaji wa ilani ,na mwenye macho aambiwi
tazama ,mbunge ni utekelezaji sio kutoa vijisenti kwa mtu mmoja mmoja.
"Sijaja
kumpigia debe Koka ila amefanya kazi ,nimeshuhudia ambulance aliyoitoa
na pikipiki na mengine mengi anayoyafanya kwa maslahi ya jamii"alisema
Mpogolo.
Awali mbunge wa
jimbo la Kibaha Mjini,Silvestry Koka alikabidhi pikipiki 14 katika kata
ambapo kila moja imegharamia milioni 2.5 na gari la wagonjwa ambalo
litasaidia katika dharura hospital ya Mkoani.
Koka
alielezea kwamba, licha ya hayo asilimia 58 ya mfuko wa jimbo
imeelekezwa katika sekta ya elimu ili kutatua changamoto za kielimu.
Wakati huo huo , alieleza
kuwa,serikali imefanya kazi kubwa kwenye sekta ya afya kwa kujenga
hospital ya wilaya na kuimarisha utawala bora ,nishati,afya,usalama na kwasasa asilimia 84 ya wakazi Jimbo la Kibaha Mjini ,wanapata maji .
Nae
mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini,Maulid Bundala alisema, wamejipanga
kushinda uchaguzi wa kata ,jimbo na Rais na kuwataka wana Kibaha wafikie
hatua ya kuwa na fadhila kwa kushukuru namna walivyoshirikiana kutatua
baadhi ya chanagamoto na mbunge kwa kipindi cha uongozi wake.
"Na
leo amekabidhi pikipiki 14 zitakazosambazwa katika kata zote na ametoa
gari la wagonjwa hospital ya Mkoani ,Tuwe na fadhila kwa kidogo
tunachopatiwa,Hatusemi kisa mseme tunamfagilia ila anapofanya mtu na
kutekeleza lazima sifa apewe"alisisitiza Bundala.
Mkuu
wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama alisema ,wanajivunia kuwa na
umoja na chama na serikali na kutekeleza ilani ya chama kwa asilimia
100.
Alieleza Koka anatosha kwani ni mengi amefanya katika Jimbo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...