Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa bendera ya Taifa jijini Dar es Salaam leo.
Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor wakiwa katika picha ya pamoja viongozi katika michezo.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia  akizungumza wakati wa kuwaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor  jijini Dar es Salaam leo, ambao wanaondoka leo jioni kuelekea nchini  Uingereza kwa ziara ya siku tatu kwenda katika klabu ya Liverpool.
 Mchezaji wa zamani, Ally Mayay Tembele  akizungumza leo na waandishi wa habari wakati wa kuwaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor ambao wanaelekea nchini Uingereza kwaajili ya kwenda kuangalia mpira nchini humo katika uwanja wa Anfield. Katikati ni Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke na Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Sandard Chartered, Sanjay Rughani.
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Sandard Chartered, Sanjay Rughani akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuwaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor ambao wataelekea nchini Uingereza kuangalia mpira katika kiwanja cha Anfield. Katikati ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia na Kushoto ni Mwalikishi wa waziri wa Habari Utamaduni na michezo, George Msonde.

 Mkurugenzi wa timu ya Dar es Salaam Corridor, Erik Kok akizungumza wakati wa kuwaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor jijini Dar es Salaam leo.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke na Kushoto akizungumza na waandishi wa haari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuwaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor na kuwapongeza kwa hatua waliyoifikia na kuwatakia safari njema. katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Sandard Chartered, Sanjay Rughani. 

Na Mwandishi wetu globu ya jamii.
BENKI ya Standard Chartered wadhamini Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor kwaajili ya kwenda katika uwanja wa Anfiel uliopo nchini Uingereza kwaajili ya kwenda kuangalia mchezo katika Uwanja huo.

akizungumza  na waandishi wa habari jiji ni Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mkuu wa  Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani  amesema kuwa wachezaji hao wataenda kujifunza mamo mbalimbali.

Amesema mbali na fursa mbalimbali watakazopata, Watanzania hao watashuhudia laivu moja ya mechi za Ligi Kuu ya England kati ya Liverpool na FC Bournemouth katika Uwanja wa Anfield nchini Uingereza.

"Mechi itachezwa Jumamosi kwenye uwanja wa Anfield," amesema na kuongeza.

"Pia watapata fursa ya kukutana na nyota wa zamani na sasa wa klabu ya Liverpool, bahati nzuri uwepo wa Samatta (Mbwana) kwenye ligi ya kule imeifanya Tanzania kujulikana, hivyo mkatumie nafasi hii kutangaza na vivutio vya Tanzania," amesema Rughani.

Kwa Upande wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amewaaga Mabingwa wa Kombe la Standard Chartered, timu ya Dar es Salaam Corridor wanaoondoka jioni ya leo kwenda Uingereza kwa ziara ya siku tatu kwenye klabu ya Liverpool.

Msafara wa timu hiyo wenye watu tisa unaondoka nchini kwenda kuishuhudia Liverpool ikikipiga na Bournemouth katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) chini ya udhamini wa benki ya Standard Chartered.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga asubuhi hii, Karia amewataka Watanzania hao kutumia vizuri fursa hiyo na kuwa mabalozi wa soka watakaporejea nchini.

"Nimeambiwa katika ziara hiyo watajifunza mambo mbalimbali kuhusu klabu ya Liverpool, uzoefu watakaoupata huko wakiutumia vema itakuwa chachu katika soka letu watakaporejea nchini.

"Naamini watajifunza miiko ya uwanja Anfield, mazingira ya klabu na nambo mbalimbali ambayo yanaihusu klabu ya Liverpool na mashabiki wake na watakaporejea itakuwa ni chachu kwao kuwapa elimu Watanzania wengine kuhusu klabu hiyo kongwe," amesema Karia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...