WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amepiga marufuku shughuli zisizohusiana na taaluma
kama ujenzi wa viwanda katika maeneo ya shule ili kutoa fursa kwa
wanafunzi kuwa kwenye mazingira mazuri ya kujifunzia.
“Sheria
inakataza kuweka matumizi yoyote yasiyokuwa ya kitaaluma katika maeneo
ya shule kwani yanasababisha kelele hivyo wanafunzi kushindwa kusoma
vizuri.”
Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni(Jumanne,
Machi 3, 2020) baada ya kupokea malalamiko ya wazazi kuhusu eneo la
shule ya msingi Mshikamano iliyoko Halmashauri ya Mji Handeni kuuzwa kwa
mfanyabiashara ambaye amefungua karakana ya kutengeneza magari.
Kufuatia
hali hiyo, Waziri Mkuu aliuangiza uongozi wa halmashauri hiyo
ukazungumze na mfanyabiashara huyo ili aondoe karakana katika eneo
hilo na kumtafutia eneo mbadala kwa ajili ya kuendesha shughuli zake na
eneo hilo libaki kwa ajili ya masuala ya kitaaluma.
Pia,
Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni upange
matumizi bora ya ardhi kwa kuainisha maeneo ya makazi, biashara, viwanda
na huduma za kijamii ili kuepuka mji huo kujengwa bila ya mpangilio.
Kadhalika,
Waziri Mkuu aliwataka wananchi kuwafikisha kwenye vyombo vya dola
walimu watakaobainika kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi.
“Serikali imeweka sheria kali ya kumlinda mtoto wa kike, ukimpa mimba,
ukimchumbia au kumuoa adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela.”
Akizungumzia kuhusu uwepo wa mabango mengi
kwenye mikutano ya hadhara ya viongozi wa Kitaifa, Waziri Mkuu alisema
kunadhihirisha wazi kwamba watendaji wa Halmashauri
hawawatembelei wananchi katika maeneo yao na kutatua kero mbalimbali
zinazowakabili.
“Watendaji
hamuendi kuwatembelea wananchi na kusikiliza matatizo yao, haiwezekani
wawe wanawasubiri viongozi wa juu na kuwasilisha kero zao, sasa
jipangeni haya mabango yote mtakuja kuyajibu kwa sababu hoja zote ni za
ngazi ya halmashauri,” alisema.
Waziri
Mkuu alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John
Magufuli imeelekeza nguvu kubwa katika kuwatumikia wananchi na kutatua
kero zao, hivyo itasimamia kuhakikisha kila mtumishi anawajibika kwa
kiwango kinachostahili.
“Serikali
hii haimlindi mfanyakazi ambaye ni mbadhilifu, mwizi na asiyefanya kazi
kwa weledi au anayebagua wananchi eti kwa uwezo wake wa kifedha au
rangi au dini yake au chama chake. Hivi vitu havipo katika Serikali kila
mwananchi aliyeko Nzega anatakiwa kuhudumiwa,”alisisitiza
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...