Mratibu wa Ugonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma wa Jiji la Dodoma, Dk Pares Lukonga akizungumza na wandishi wa habari leo ikiwa ni maadhimisho ya ugonjwa huo.

Charles James, Globu ya Jamii
KUTOKANA na kuwa na kinga dhaifu makundi ya wazee, watoto na watu wenye magonjwa ya kurithi wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu.

Akizungumza jijini Dodoma leo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani, Dk Peres Lukango ambaye ni mratibu wa kifua kikuu na ukoma ngazi ya jiji Dodoma amesema miili ya makundi hayo kinga yake ni ndogo kulinganisha na makundi mengine.

Amesema makundi ya wazee huwa kwenye hatari ya kupata maambukizi ya Kifua kikuu kwa sababu  kinga ya mwili hushuka kutokana na umri kusonga mbele lakini watoto hukumbana na hatari hiyo kutokana na uchanga wao na mifumo yao ya kinga inakua haijakomaa.

Dk Lukango amesema jiji la Dodoma hawako nyuma katika kupambana na ugonjwa huu ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu visabanishi vya ugonjwa huo na hatua gani wanapaswa kuchukua ili kuweza kuepukana nao.

" Jiji la Dodoma tunayo mikakati mingi ya kukabiliana na ugonjwa huu, mikakati yetu ipo katika kuwatafuta, kuwafikia, kuwachunguza watu wenye maambukizi ya ugonjwa huo na kama ikithibitika wameambukizwa kifua kikuu ni kuwahi kwenye huduma ya matibabu na kuhakisha kuwa  wanaanza dozi mapema.

" Kipindi cha nyuma tulikuwa tunafanya kazi hii kwa kusubiri wagonjwa waje kwenye vituo vya afya lakini kama mtu yuko nyumbani kwake anakohoa leo, kesho akaenda duka la dawa, akanunua dawa,akaenda kwa waganga lakini imefika mahali sasa wanatoka huko walipo wanakuja vituo vya afya kwaajili ya kupata ushauri wa kitalaamu’’ Dkt lukango

Kwa upande wake Phoibe Nhonya ni muuguzi katika kituo cha kupambana na ugonjwa huo amesema wamekuwa wakihudumia wagonjwa wa kifua kikuu kwa kuwapa dawa ambazo hutumia kwa miezi sita huku Rose Lema ambaye ni muhudumu wa afya ngazi ya jamii akisema kuwa wamekuwa wakiwafuatilia wale wagonjwa ambao wameanza tiba ili wasiache na kuhudhuria kliniki inavyotakiwa kwani wakiacha dawa watakuwa na TB sugu.

Nae Nelson Mathias ambaye ni Mwananchi wa Jiji la Dodoma amesema bado kumekuepo na changamoto ya elimu kwa wananchi wengi katika kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo na kutoa rai kwa serikali kuongeza spidi ya utoaji elimu.

"Jamii zetu bado zina uelewa mdogo sana katika kukabiliana na ugonjwa huu, hatari yake ni kubwa pindi mgonjwa mmoja anapopata maambukizi kwani ni rahisi kuambukiza wengine. Niwaombe wataalamu wetu na serikali zizidishe utoaji elimu," Amesema Mathias.

Maadhimisho ya siku ya kifua kikuu hufanyika kila Machi 24 ya kila mwaka na mwaka huu yanaenda sambamba na kauli mbiu isemayo, " Wakati ni huu tuunganishe nguvu na kuwajibika katika mapambano dhidi ya Kifua Kikuu."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...