Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway amesema kuwa, Umoja wa Mataifa utaanzisha mfuko wa kusaidia matibabu ya wagonjwa wa virusi vya corona katika pembe mbalimbali za dunia.
Taarifa iliyotolewa na Ine Eriksen Søreide imesema kuwa, mfuko huo utazishirikisha jumuiya na taasisi wafadhili chini ya Umoja wa Mataifa kwa shabaha ya kuzidisha juhudi za kimataifa za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona na kuwasaidia watu walioambukizwa virusi hivyo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, tangazo rasmi la kuasisiwa mfuko huo litatolewa siku chache zijazo na kwamba lengo lake ni kuzisaidia nchi zinazostawi ambazo zina mifumo dhaifu ya matibabu kwa ajili ya kukabiliana na mgogoro wa corona.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway amesema kuwa, lengo jingine la kuanzishwa mfuko huo ni kukabiliana na taathira za muda mrefu za maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 (corona).
Hadi sasa zaidi ya watu 351,426 wameambukizwa virusi vya corona katika nchi mbalimbali duniani na 15,361 miongoni mwao wameaga dunia kutokana na virusi hivyo.
Idadi kubwa zaidi ya maambukizi na vifo vya watu kutokana na virusi vya corona inashuhudiwa katika nchi za Magharibi kama Italia, Uhispania, Ufaransa na Marekani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...