Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.
WAFUASI na viongozi 27 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamefikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya kutoa maneno ya maudhi kwa askari magereza na kuharibu geti la gereza la Segerea.
Hata hivyo ni washtakiwa 15 tu ndio wamesomewa mashtaka yao leo Machi 23,2020. Hata hivyo upande wa mashtaka umeomba hati ya wito kwa washtakiwa 12 ambao hawakuwepo leo mbele ya mahakama kujibu mashtaka yao ili waweze kuletwa na kusomewa mashtaka yao.
Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali Mwandamizi Renatus Mkude amewataja washtakiwa hao kuwa ni Halima Mdee Mbunge wa Kawe, Ester Bulaya Mbunge wa Bunda Mjini, Jesca Kishoa Mbunge wa viti Maalimu mkoa wa Singida na Boniphace Jacob Meya wa Ubungo na Diwani wa Chadema Patrick Assenga.
Wengine ni, Henry Kilewo, Yohana Kaunya, Mshewa Karua, Angela Tryphone, Khadija Mwango, Reginald Masawe , Pendo Raphael, Cesilia Michael, Happy Abdallah, Paulo Makali.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi imedaiwa kuwa, Machi 13 mwaka huu, huko katika Gereza la Segera lililoko ndani ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao wote isivyo halali na kwa makusudi walikaidi amri iliyotolewa na Afisa wa magereza mwenye namba D 3648 Sajenti John iliyowataka kuondoka eneo hilo kwa amani na kuacha eneo hilo salama wakati alipokuwa akitimiza majukumu yake ya kazi ambae alikabidhiwa kulinda geti kuu la ngome ya Segerea.
Katika shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo washtakiwa hao walikusanyika isivyo halali na kusababisha hali isivyo ya kawaida kwa jirani waliokuwa pale hali iliyopelekea hofu kuleta hofu na kuhatarisha amani na utulivu .
Washtakiwa hao pia wanadaiwa kwa pamoja walishirikiana kufanya uharibifu katika geti Kuu linaloingia gereza la Segera, geti ambalo ni mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha katika shtaka la nne na la tano washtakiwa Bulaya na Mdee wanadaiwa kutoa maneno ya kuudhi kwa Sajenti John maneno ambayo yalipelekea uvunjifu wa amani.
Aidha Mshtakiwa Jacob anadaiwa kuwa siku na mahali hapo alitamka maneno ya kuudhi kwa Sajent John na pia anadaiwa kumfanyia shambulio Sajenti huyo kwa kumkunja na kumvuta shati askari huyo wakati akitekeleza majukumu yake hali iliyopelekea shati hilo kuchanika.
Hata hivyo washtakiwa wote wamekana kutenda makosa hayo na wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa ambayo kila mmoja wametakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua ya utambulisho atakayesaini bondi ya sh. Milioni nne.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umeishakamilika na imeahirishwa hadi Aprili 23 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...