Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
ANNAMARIA
Jose Raphael Gonzales (34) raia wa Mexico ambaye pia alikumbwa na
virusi vya Corona (Covid -19) amejifungua mapacha na kuwaita Corona na
Virus mtandao wa World News, Daily report umeripoti.
Imeelezwa
kuwa Annamaria alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya La Villa
mjini Mexico na kujifungua mapacha hao wenye afya tele ambapo mtoto wa
kike amepewa jina la Corona Jose Miguel Gonzales na kaka yake ameitwa
Virus Jose Miguel Gonzales.
Annamaria ameeleza kuwa;
"Sikuwa
na jina nililopanga kuwaita, mmoja wa madaktari alishauri niwaite
Corona na Virus kwa kuwa niliathirika na virusi hivyo, nikaona na wazo
zuri" ameeleza.
Daktari
Eduardo Castillas kutoka hospitali hiyo alivieleza vyombo vya habari
kuwa alipendekeza majina hayo kwa utani tuu, ila wanashukuru mama na
watoto hao wanaendelea vizuri.
"Nilimwambia awaite Corona na Virus kama utani lakini akamakinikia" ameeleza Dkt. Eduardo huku akicheka.
Annamaria alitarajia kwenda kujifungua nchini Marekani wiki ijayo lakini hakufanikiwa kuvuka mpaka.
Mwaka
2017 mwanamke mmoja kutoka Mexico alimpa mwanaye jina la Malaria baada
ya kupimwa na kugundulika kuwa na vimelea hivyo, na mwaka 2018 mwanamke
mwingine alimpa binti yake jina la Gonorrea baada ya kukumbwa na
magonjwa ya zinaa kwa vipindi mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...