MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh.
Saleh Omar Kabi,akiongoza dua Maalum ya kuiombea Nchi kutokana na
Maradhi ya Corano,iliofanyika kwa njia ya vyombo vya habari katika
ukumbi wa ZBC Karume House Zanzibar jana usiku na kuoneshwa moja kwa
moja, (kushoto kwa Mufti) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Hassan
Othman Ngwali na ( kulia kwa Mufti) Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar.Sheikh.
Mahmoud Mussa Wadi, wakiwa na masheikh wengine wakiitikia dua hiyo
iliofanyika jana usiku.(Na.Othman Maulid) 

SHEIKH Dkt. Muhidin Ahmady (Mwalim
Siasa) akisoma dua wakati wa Dua Maalum ya kuiombea Nchi kutokana na
Maradhi ya Corona (CODIV -19) kulia Sheikh Shaban Ali Batashi, Mshauri
wa Waziri wa Sheria na Katiba Sheikh Fadhil Soraga na Sheikh. Said
Suleiman wakiitikia dua hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa ZBC Karume
house jana usiku.(Picha na Othman Maulid).

MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh
Saleh Omar Kabi akisoma dua maalum ya kuiomba Nchi kutokana na Maradhi
ya Corona, iliyofanyika kupitia vyombo vya habari vya ZBC TV na Redio na
kurushwa moja kwa moja kwa wananchi, (kushoto kwa Mufti) Naibu Kadhi
Mkuu wa Zanzibar.Sheikh. Hassan Othma Ngwali na (kulia kwa Mufti) Naibu
Mufti Mkuu wa Zanzibar.Sheikh Mahmoud Mussa Wadi, wakiitikia dua hiyo,
ilioyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha ZBC mnazi mmoja Jijini Zanzibar
jana usiku.(Picha na Othman Maulid)

SHEIKH Abdulraham Sheikh Al-Habshi
akisoma dua maalum ya kuiombea Nchi kutokana na Maradhi ya Corona
iliyofanyika kupitia chombo cha habari cha ZBC TV na Redio na kurushwa
moja kwa moja jana usiku, (kushoto kwake)Sheikh. Samir Zukfika Ramdhan
na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume.(Picha na
Othman Maulid)

NAIBU Kadhi Mkuu wa Zanzibar
Sheikh. Hassan Othman Ngwali akisoma dua wakati wa hafla ya kuiombea
Nchi Dua ya kutokana na Maradhi ya Corona yalioikumba dunia, dua hiyo
imefanyika kwa njia ya Vyombo vya Habari vya ZBC Tv na Redio, katika
kituo hicho Karume House Mnazi mmoja Jijini Zanzibar, (kulia) Mufti Mkuu
wa Zanzibar. Sheikh Saleh Omar Kabi na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar
Skheih Mahmoud Mussa Wadi.(Picha na Othman Maulid)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...