Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Gerald Mweli akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga alipofika wilayani hapo kwa ziara yake ya kikazi.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Gerald Mweli akitoa maelekezo kwa baadhi ya viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali.
NAIBU Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu OR-TAMISEMI Gerald Mweli ametembelea halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na kukagua eneo la ujenzi wa Ofisi ya Utawala itakayoanzwa kujengwa katika Eneo hilo hivi karibuni.
Halmashauri hiyo ambayo hapo awali Ofisi zake zilikua katika eneo la Utawala la Shinyanga Manispaa wamehamia katika eneo hilo baada ya Agizo la Rais Mh Dkt John Magufuli lililotolewa Mwezi Oktoba, 2020 la kuzitaka Halmashauri zote zihamie katika maeneo yao ya Utawala.
Akizungumza baada ya kuona eneo la ujenzi lenye ukubwa wa Ekari 20 lililoko katika eneo la Isela Maganzi Mweli amesema amekuja kujiridhisha endapo eneo limeshapatikana na liko sehemu salama.
" Hapa nimeridhika eneo ni zuri lina ukubwa wa kutosha na litatosha kwa ujenzi wa Ofisi na maendeleo mengine ya Halmashauri hapo baadae’ Amesema Mweli.
Aidha Mweli alipata nafasi ya kukutana na Menejimenti ya Shinganya Dc na kupata taarifa ya ukusanyaji aa mapato pamoja na utoaji wa mikopo kwa vikundi.
Akiwasilisha taarifa ya mapato Kaimu Mkurugenzi wa Shinyanga DC amesema makusanyo mpaka kufikia robo ya Pili waliweza kufikia asilimia 30% tu ya lengo walilojiwekea na hii ni kutokana na mapato yao kutegemea zao la pamba ambalo kwa kipindi hicho hali yake haikuwa nzuri.
Pia aliongeza kuwa mikopo iliyotolewa kwa vikundi 8 katika robo ya kwanza ni shilingi Mil. 28 na hivi karibuni watatoa shilingi milioni 56 kwa vikundi 5 ambavyo vimepitishwa.
Mweli alitoa angalizo kuwa ukusanyaji wa mapato hauridhishi hata kidogo na kusisitiza kama mapato hayo yanategemea mazao basi waongeze nguvu katika vyanzo vingine ambavyo havitegemei hali ya hewa na kuhakikisha vinakusanywa kwa asilimia 100.
Mweli alimalizia kwa kuwataka Halmashauri ya hiyo kuanza kupima maeneo ya makazi, biashara na Taasisi ili kupanga makao makuu ya Wilaya hiyo na kuendana na kasi ya ukuaji wa mji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...