Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewataka wafanyakazi wa umoja huo kufanyia kazi nyumbani kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na hatari ya kuenea ugonjwa wa COVID-19 (corona).
Kwa mujibu wa taarifa, siku ya Ijumaa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuanzia 16 Machi hadi 12 Aprili wafanyakazi wa makao makuu ya umoja huo mjini New York watafanyia kazi zao nyumbani isipokuwa tu wale ambao ni dharura wafike ofisini.
Tangazo hilo limetolewa baada ya mwanadiplomasia wa Ufilipino katika umoja wa huo kupatikana na kirusi cha Corona. Mwanadiplomasia huyo alikuwa ameshiriki moja ya vikao vya Umoja wa Mataifa.
Wakati huo huo, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric ametangaza kuwa kuanzia tarehe 16 Machi hadi mwisho wa mwezi Aprili vikao vingi vya kando vilivyokuwa vifanyike kwenye makao makuu sasa vimesitishwa. Ameongeza kuwa Katibu Mkuu António Guterres amezijulisha nchi wanachama na maafisa mbalimbali kwamba mikutano yote ya kando kuanzia Machi 16 hadi mwisho wa Aprili kwenye makao makuu mjini New York imefutwa.
Ziara za kuzuru makao makuu ya Umoja wa Mataifa zinazofanywa na umma kila siku pia zimesitishwa na usafi mkubwa unazingatiwa ikiwa ni pamoja na kuongeza kemikali za kuuwa vijidudu kwa kusafisha mikono.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...