Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Katika kuelekea uchaguzi Mkuu 2020 wa Rais, Wabunge na madiwani Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekutana na viongozi wa vyama vya siasa kujadili maandalizi ya uwekaji wazi wa Daftari la awali na kutoa taarifa ya maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili.
Akifungua mkutano huo uliohusisha viongozi wa vyama vya siasa nchini Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage amesema katika kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu uandikishaji wa wapiga kura na uwekaji wazi wa Daftari la awali la mpiga kura ni muhimu.
Aidha amesema uwekaji wazi wa wa daftari la kudumu la wapiga kura utafanyika kwa mujibu wa vifungu vya 11A MA 22 vya sheria ya Taifa ya uchaguzi na kifungu cha 15A cha sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa ambapo tume inatakiwa kuweka wazi daftari la awali ili kutoa fursa kwa wananchi kulikagua na kuhakiki taarifa zao.
Jaji Kaijage amesema uhakiki huo unaenda na marekebisho pale inapohitajika ambapo lengo lingine la uwekaji wazi daftari hilo ni pamoja na kuwaondoa watakaothibitika kukosa sifa baada ya kuwekewa pingamizi.
" Zoezi la uwekaji wazi daftari litawahusu si tu Wale walioandikishwa katika uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura kwa awamu ya kwanza bali pia wapiga kura wote walioandikishwa mwaka 2015"Amesema Jaji Mstaafu Kaijage.
Sambamba na hayo amesema katika kuhakikisha kuwa kila mpiga kura aliyeandikishwa anapata nafasi ya kuhakiki taarifa zake Tume imeweka njia 3 tofauti zitakazotumika ikiwemo ni kufika kwenye vituo walivyojiandikishia, kutumia mfumo wa Voters Interaction systems (VIS) kwa kupitia simu na kupiga *152*00# na kufuata maelekezo.
Aidha ameongeza kuwa jumla ya wapiga kura waliopo katika Daftari la awali kwa sasa ni zaidi ya milion 30 ambapo idadi hiyo inaweza kubadilika baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki na uchakataji wa taarifa za wapiga kura endapo watabainika waliojiandikisha zaidi ya mara moja.
Hata hivyo amesema Tume inaendelea kuwasisitiza wananchi kujitokeza kwenda kuhakiki taarifa zao daftari litakapowekwa wazi katika maeneo yao na wasisite kuwawekea pingamizi wapiga kura wasio na sifa za kuwemo kwenye daftari ili kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Dkt Wilson Mahera amesema sifa za mtu anaetakiwa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ni mtanzani mwenye umri wa miaka 18 na kuendele na wasio na sifa ni asie raia wa Tanzania aliyehukumiwa adhabu ya kifo, mgonjwa wa akili hao wote hawastahili kuingia kwenye daftari la kudumu la mpiga kura.
Akichangia mada katika Mkutano Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi John Shibuda amesema kuwa na ushirikiano wa karibu kati NEC na vyama vya siasa.
Amesema kamatakamata kwa viongozi wa siasa sio sawa kutokana na baadhi ya watu kukosa taarifa.
Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Dkt Wilson Mahera amesema sifa za mtu anaetakiwa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ni mtanzani mwenye umri wa miaka 18 na kuendele na wasio na sifa ni asie raia wa Tanzania aliyehukumiwa adhabu ya kifo, mgonjwa wa akili hao wote hawastahili kuingia kwenye daftari la kudumu la mpiga kura.
Akichangia mada katika Mkutano Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi John Shibuda amesema kuwa na ushirikiano wa karibu kati NEC na vyama vya siasa.
Amesema kamatakamata kwa viongozi wa siasa sio sawa kutokana na baadhi ya watu kukosa taarifa.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage akizungumza na viongozy wa vyama vya siasa nchini katika kuelekea Uchaguzi Mkuu na masuala mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa daftari la kudumu la Mipiga kura.
Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya Siasa John Shibuda akichangia mada katika Mkutano wa viongozi wa vyama Siasa na NEC uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uchazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt.Wilson Mahera akitoa mada kwa viongozi wa vyama vya siasa katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Mratibu Uhamasishaji wa Elimu ya Afya kwa Jamii wa Ofisi ya Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala Sophia Ntomola akitoa maelezo ya kujinga na Virusi vya Corona katika Mkutano kati ya NEC na Vyama vya Siasa katika kuchukua tahadhari zaidi za kujikinga.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Dkt.Wilson Mahera akimkabidhi kitabu Cha uboreshaji wa daftari la kudumu la Mipiga kura awamu ya kwanza Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Chauma Eugene Kabendera wakati wa Mkutano kati ya NEC na Viongozi ea vyama vya Siasa.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Dkt. Wilson Mahera akimkabidhi kitabu Cha uboreshaji wa Daftari la Mipiga Kura awamu ya kwanza Mkurugenzi wa Oparesheni na Mafunzo wa Chadema Benson Kigaila katika Mkutano kati ya NEC na Vyama vya Siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...