Na Woinde Shizza, ARUMERU
Wajumbe
wa baraza la madiwani Halmashauri ya Meru, wilayani Arumeru,
wamekubaliana kuwa na agenda ya kutokomeza mimba za utotoni na utoro
shuleni kudumu kwenye vikao vya Vijiji na Kata kwa kujikita kuelimisha
jamii kuanzia ngazi ya familia.
Wajumbe
hao wameadhimia hilo, mara baada ya, madiwani wa Kata kadhaa
kuwasilishwa taarifa zinazoonesha changamoto ya mimba za utotoni
zinazowaka bili wanafunzi katika kata zao.
Awali
taarifa hizo zimethibitishwa na Idara ya Elimu Msingi na Sekondari
kuthibitisha kuwa jumla wanafunzi 67 wamepata mimba kwa mwaka
2017/2018.
Afisa
elimu Sekondari Mwl Emmy Mkuru alieleza kuwa kwa kipindi cha Mwezi Januari 2017 mpaka sasa jumla ya wanafunzi 57 waliripotiwa kupata mimba
ambapo kati yao wanafunzi 27 wamepata mimba kuan zia mwezi Januari
mwaka huu 2018.
Mwl.Emmy
ametoa rai kwa wazazi kutekeleza jukumu la malezi kwa wanafunzi
sambamba na kujenga mabweni ili kuwaepusha wanafunzi hao wa kike na
vishawishi wanavyokutana navyo kwa kutembea umbali mrefu kwenda shule .
Nae
mwakilishi wa Afisa elimu Msingi Makius Ngazi alieleza kuwa kwa
kipindi cha Mwezi Januari Mwaka 2017 hadi Mwezi Octoba mwaka huu jumla
ya wanafunzi 10 wa shule za Msingi wamepata mimba na kushindwa kuendelea
na Masomo.
Mwanasheria
wa Halmashauri hiyo,wakili Magdalena John alisema Serikali iliweka
sheria ili kumlinda Mwanafunzi kutokukosa fursa ya masomo ila
changamoto kubwa katika kushughulika na kesi za mimba kwa wanafunzi ni
utoaji wa ushahidi hivyo ametoa rai kwa wazazi na jamii kutoa ushahidi
kwa wakati.
Makamu
mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Nelson Mafie amesikitishwa na wazazi
kutokua mstari wa mbele kutoa taarifa za wanafunzi kupata mimba na
kusubiri viongozi kuja kuzitafuta. "tumeona hivi karibuni Mkuu wetu wa
Wilaya Jerry Muro akipambana kutokomeza mimba kwa wanafunzi kwa
kuwachukulia hatua wahusika , hivi wazazi na jamii tunakuwa tupo wapi ?'
" Alihoji Mafie .
"Halmashauri imejipanga vipi kumaliza swala la mimba kwa wanafunzi ?"amehoji Diwani viti maalumu Kata ya Usa -River Meri Antony
Akihitimisha
mjadala huo mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Will Njau, ametoa rai kwa
viongozi wa dini ,mila na siasa kutoa elimu huku muongozo wa baraza hilo
agenda ya kutokomeza mimba za utotoni kwa wanafunzi na utoro kuwa ya
kudumu katika vikao ngazi za vijiji na kata .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...