MAKAMANDA wa JWTZ wakiwa wamebeba jeneza la mwili wa Marehemu Ramadhani Haji Faki wakiingia katika viwanja vya Masjid Mushawar Muembeshauri Wilaya ya Mjini Unguja kwa ajili ya kuusala na kuuombea dua

NDUGU na Jamaa wa Marehemu Ramadhan Haji Faki Waziri Kiongozi Mstaaf wa Zanzibar, wakiwa wamebeba jeneza likiwa na mwili wa marehemu wakiingia katika Masjid Mushawar Muembeshauri Wilaya ya Mjini Unguja kwa ajili ya kumuombea marehemu.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akijuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika Sala ya kumuombea Marehemu Ramadhan Haji Faki Waziri Kiongozi na Bregedia Jeneral Mstaaf, ikiongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar. Sheikh. Saleh Omar Kabi, iliofanyika katika Masjid Mushawar Muembeshauri Wilaya ya Mjini Unguja, leo 29-3-2020.,

BAADHI ya Viongozi na Wananchi wakishiriki katika Ibada ya Sala ya Maiti kumuombea Marehemu Ramadhan Haji Faki, iliofanyika katika Masjid Mushawar Muembeshauri Wilaya ya Mjini Unguja leo,29-3-2020.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,.Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam wakiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika Sala ya kuuombea mwili wa Marehemu Ramadhan Haji Faki , iliofanyika katika Masjid Mushawar Muembeshauri Wilaya ya Mjini Unguja leo, 29-3-2020

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Kassim Majaliwa, wakisubiri kuwasili kwa mwili wa Marehemu Ramadhan Haji Faki, kijiji kwao Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa ajili ya hafla ya maziko hayo yaliofanyilka leo 29-3-2020.

BAADHI ya Wananchi wakihudhuria hafla ya maziko ya Waziri Kiongozi Mstaaf na Brigedia Jenerali Mstaaf Ramadhan Haji Faki yaliofanyika Kijiji kwao Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini Unguja leo.29-3-2020.

MAKAMANDA wa JWTZ wakiwa wamebeba jenela la mwili wa Marehemu Ramadha Haji Faki wakielekea katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya maziko katika Kijiji chao Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja yaliofanyika leo,29-3-2020.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein (kulia kwa Rais) Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na ( kushoto kwa Rais) Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar.Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo, wakiwa katika maziko ya Marehem,u Ramadhan Haji Faki, Waziri Kiongozi na Brigedia Jenerali Mstaaf, yaliofanyika Kijiji kwao Mkwajuni Mkoa wa Kaskaziuni Unguja leo.29-3-2020.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Ramadhan Haji Faki, wakati wa hafla hiyo ya maziko yaliofanyika katika Kijiji cha Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.

WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Ramadhan Haji Faki, wakati wa hafla hiyo ya maziko yaliofanyika katika Kijiji cha Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.

MKUU wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo, akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Ramadhan Haji Faki, wakati wa hafla hiyo ya maziko yaliofanyika katika Kijiji cha Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Kassim Majaliwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na Wananchi wakiitikia dua ikisomwa baada ya kumalizika kwa maziko ya Marehemu Ramadhani Haji Faki, yaliofanyika Kijiji cha Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 29-3-2020.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapiunduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein (kulia kwa Rais) Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe Kassim Majaliwa na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar. Brigedia Jenerali.Fadhil Omar Nondo, wakiwa wameshima wakati ikipingwa mizinga 17, wakati wa hafla ya maziko ya Brigedia Jenerali Mstaaf na Waziri Kingozi Marehemu Ramadhan Haji Faki yaliofanyika kijiji kwao Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 29-3-2020

ASKARI wa JWTZ wakitowa heshima wakati wa hafla ya maziko ya Marehemu Ramadhan Haji Faki Birigedia Jenerali Mstaaf yaliofanyika Kijiji kwao Mkoa wa Kaskazini Unguja.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akitowa wasifu wa Marehemu Waziri Kiongozi Mstaaf na Brigedia Jenerali Mstaaf. Ramadhan Haji Faki, yaliofanyika katika kijiji kwao Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.29-3-2020.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasalimia na kuwafariji Ndugu na Jamaa wa Marehemu Ramadhan Haji Faki, baada ya kumalizika kwa maziko yaliofanyika kijiji kwao Mkwajuni Mkoa wa Kaskaziniu Unguja leo 29-3-2020.(Picha na Ikulu)
======= ====== ========
======= ====== ========
DKT. SHEIN AONGOZA MAZISHI YA WAZIRI KIONGOZI MSTAAFU WA ZANZIBAR.
- MAJALIWA AMWAKILISHA JPM KATIKA MAZISHI HAYO
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed
Shein leo amongoza waombolezaji katika mazishi ya Waziri Kiongozi
Mstaafu wa Zanzibar, Brigedia Jenerali Mstaafu, Ramadhani Haji Faki
yaliyofanyika Mkwajuni Zanzibar.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe
Magufuli katika mazishi hayo, alipata fursa ya kutoa salamu za pole za
Rais kwa wanafamilia na ndugu wa marehemu baada ya mazishi .
Akitoa
salamu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Waziri wa Nchi , Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Abood amemuelezea
marehemu kuwa ni kiongozi aliyekuwa mstari wa mbele kutetea haki na
kusimamia maendeleo katika nchi yetu.
“Aliweka
mbele maslahi ya taifa na kuweka mbali maslahi yake binafisi ndiyo
maana alishiriki katika vita kati ya Tanzania na Uganda vilivyomundoa
madarakani Nduli Iddi Amini.”
Marehemu
alizaliwa mwaka 1930 katika kijiji cha Mkwajuni, Kaskazini Unguja na
mwaka 1983 hadi 1984 alikuwa ni Waziri Kiongozi wa Zanzibar.
Wakati
huo huo, Waziri Mkuu leo ametoa pole kwa familia ya Waziri
Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine ambayo
imeondokewa na Lazaro Edward Sokoine, aliyefariki Machi 28,2020
katika hospitali ya taifa Muhimbili alikokuwa akitibiwa.
Kwa
mujibu wa msemaji wa familia Balozi Joseph Sokoine ambaye Pia ni Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, kesho kutakuwa na misa ya
kumuombea marehemu kwenye kanisa katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro,
Oysterbay jijini Dar es salaam.
Amesema mazishi yanatarajiwa kufanyika katika kijiji cha Embwiki Monduli Juu keshokutwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...