
RAIS wa
Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein ,
akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji
Zanzibar, wakati wa kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa
Wizara hiyo kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 , mkutano uliofanyika
Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, (kulia kwa Rais) Katibu Mkuu Kiongozi
na Katibu wa Baraza la Mapinduzi. Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na Waziri
wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Dr. Sira Ubwa


BAADHI ya
Wakurugenzi wa Idara na Mashirika mbalimbali yal Wizara hiyo
wakifuatilia uwasilishwaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa
mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 /2020, mkutano uliofanyika ukumbi wa
Ikulu Jijini Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo pichani)

WAZIRI wa
Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Dr. Sira Ubwa akisoma muktasari
wa taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara yake kwa mwezi wa
Julai hadi Disemba 2019 /2020, mkutano uliofanyika ukumbi wa Ikulu
Jijini Zanzibar, (kushoto) Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la
Mapinduzi. Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee.

KATIBU Mkuu
Wizara ya Ujenzi Mawasiliani na Usafirishaji Ndg. Mustafa Aboud Jumbe,
akisoma Taarifa ya Utekelezaji ya Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai hadi
Disemba 2019/2020, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini
Zanzibar.

MKURUGENZI
Idara ya Usafiri na Leseni Zanzibar. Ndg. Suleiman Konoo Kirobo,
akijibu swali wakati wa Mkutano wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji
mpango Kazi kwa mwezi Julai hadi Disemba 2019 /2020, kiongozwa na Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein.(hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini
Zanzibar.


BAADHI ya
Maofisa wa Idara na Mashirika ya Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na
Usafirishaji wakifuatilia uwasailishwaji wa utekelezaji wa Mpango Kazi
wa Wizara hiyo ukiwasilishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano
na Usafirishaji Ndg. Mustafa Aboud Jumbe,(hayupo pichani) mkutano huo
umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

KATIBU wa Bodi
ya Usafiri Zanzibar Ndg. Mohammed Simba Hassan, akijibu swali liliolizwa
wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai hadi
Disemba 2019/2020, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein. (hayupo pichani)

MKURUGENZI Mkuu
wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini (ZMA).Capt. Abdalla Hussein Kombo,
akijibu swali wakati wa mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji ya
Mpango kazi kwa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji
uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, ukiongozwa na Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, (hayupo pichani)

MKURUGENZI Mkuu
wa Shirika la Bandari Zanzibar Ndg. Abdalla Juma, akijibu swali wakati
wa mkutano wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji Mpango Kazi kwa mwezi
wa Julai hadi Disemba 2019/2020 , ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo
pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na
Ikulu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...