Na Ripota  Wetu, Michuzi Globu

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanaharakati Wazalendo Siasa Tanzania(UWASAT) umevitaka vyama vya upinzani nchini kuwa makini na aliyekuwa kada wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Bernard Membe ambaye kwa sasa amefukuzwa kwenye Chama hicho.

Kwa mujibu wa UWASAT ni kwamba huenda Membe ameondolewa CCM kama mtego kwa wapinzani na hivyo iwapo wataamua kumchukua inaweza kusababisha upinzani nchini kumalizwa kwa urahsi zaidi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Umoja huo Kunje Ngombale Mwiru amesema wapinzani ni vema wakawa makini na Membe huku akifafanua kuwa yasije yakatokea kama ya mwaka 2015 ambapo wapinzani waliwachukua makada wa CCM na leo hii wote wamerudi na siri lukuki za upinzani.

"CCM ni familia moja na hivyo lazima wapinzani wawe makini sana, wawe makini na Membe kwani lisije likatokea kama la mwaka 2015,kwani unaweza kukuta kategeshwa ili wapinzani wamchukue ili aje kuvimaliza vyama vya upinzani,"amesema Kunje.

Ameongeza kuwa yeye amekuwa muumini wa ukweli kwa miaka yote na kwamba uchaguzi wa mwaka 2015 kabla ya kesho yake kwenda kuchagua viongozi,aliwaambia Watanzania kuwa watu waliotoka CCM na kwenda upinzani hawataweza kuleta mabadiliko."Na sasa mnajionea wenyewe wote wamerudi kundini."

Wakati huo huo amesisitiza kuwaUWAST hakitawafumbia macho viongozi wanasiasa wenye kutoa ahadi za uongo na zisizotekelezeka kwa wananchi.

Kunje amesema wapo tayari kuendelea kueleza ukweli kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea nchini na hasa kwenye masuala ya kisiasa na kuongeza watakuwa tayari tamko lolote kuhusu mambo yanayohusu nchi na Afrika kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...