Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imesema imevunja mkataba baina ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Kampuni ya ROM Solution Co. Ltd ambao ulikua wa ununuzi wa vifaa vya jeshi hilo wenye thamani ya zaidi ya Shilingi Trilioni moja.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe George Simbachawene leo jijini Dodoma ambapo amesema makubaliano hayo yalishavunjwa na pande zote mbili kuridhia na wala hakuna hasara yoyote iliyojitokeza wala madai yoyote ambayo serikali imeyapata.

Januari 23 wakati Rais Dk John Magufuli akizindua nyumba za askari wa Magereza Ukonga alielekeza kufanyika kwa uchunguzi wa juu ya mkataba baina ya jeshi hilo la Zimamoto na Kampuni  hiyo baada ya kueleza kutoridhishwa na makubaliano ya mkataba yaliyokuepo.

"Kama mnakumbuka Januari 27 mwaka huu wakati Mhe Rais Magufuli ananiapisha Ikulu aliniagiza pia kushughulikia suala la mkataba tata kati ya Jeshi la Zimamoto na Kampuni hii ya ROM.

Katika kushughulikia suala hili nimebaini kuwepo kwa hati ya makubaliano yaliyoingiwa Agosti 22 mwaka 2019 kati ya aliyekua Kamishna Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa niaba ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Kampuni ya ROM. Hati hiyo ya makubaliano ilikua ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya jeshi hilo vyenye thamaninya Euro 408,416,238.16 kulingana na thamani iliyoainishwa katika andiko la mradi husika," Amebainisha Mhe Simbachawene.

Amesema baada ya Serikali kupitia hati hiyo iliyoingiwa na Jeshi la Zimamoto na Kampuni hiyo iliona haina haja ya kuendelea na makubaliano husika juu ya mradi uliokusudiwa kwani haukua na tija kwa Nchi na hivyo kuamua kuvunja makubaliano hayo tangu Februari mwaka huu.

Makubaliano ya mkataba huo ndio yaliyosababisha kutumbuliwa kwa aliyekua Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola pamoja na aliyekua Kamishan wa Jeshi hilo Thobias Andengenye. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe George Simbachawene akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dodoma kuhusu kuvunjwa kwa mkataba baina ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Kampuni ya ROM Solution.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Simbachawene amesema Serikali imevunja Mkataba na Kampuni ya Rom Solutions ya Nchini Romania ambao ulihusu ununuzi wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa gharama ya Euro 408,416,288.16, ambazo ni sawa na Shilingi Trilioni moja. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati), akimsikiliza Mwandishi wa Habari wa gazeti la Habari leo, Mroki Mroki alipokuwa anamuuliza swali katika Mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika, ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Simbachawene amesema Serikali imevunja Mkataba na Kampuni ya Rom Solutions ya Nchini Romania ambao ulihusu ununuzi wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa gharama ya Euro 408,416,288.16, ambazo ni sawa na Shilingi Trilioni moja.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Simbachawene amesema Serikali imevunja Mkataba na Kampuni ya Rom Solutions ya Nchini Romania ambao ulihusu ununuzi wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa gharama ya Euro 408,416,288.16, ambazo ni sawa na Shilingi Trilioni moja. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio. Picha
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Simbachawene amesema Serikali imevunja Mkataba na Kampuni ya Rom Solutions ya Nchini Romania ambao ulihusu ununuzi wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa gharama ya Euro 408,416,288.16, ambazo ni sawa na Shilingi Trilioni moja. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...